Joe Biden ameonya Urusi dhidi ya kuendelea kudhibiti mji wa Crimea
Makamu
wa Rais wa Marekani Joe Biden amesema sharti Urusi ikome kuongea sana
na badala yake ianze kufanya kazi ya kusitisha mgogoro wa kisiasa nchini
Ukraine.
Bwana Biden aliyasema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo waziri mkuu wa Ukraine Arseniy Yatsenyuk pia alihudhuria.
Marekani imeonya Urusi kuwa ikiendelea kuchochea hali nchini Ukraine , itatengwa na jamii ya kimataifa. Pia ameitaka Urusi kukomesha uungaji mkono wa vikosi vya Ukraine vinavyounga mkono Urusi.
Joe Biden, amesema kuwa Marekani iko tayari kuwasaidia viongozi wa Ukraine kufikia kile alichokitaja kuwa fursa ya kihistoria ya kujenga taifa la Ukraine lenye umoja.
Biden pia aliwahutubia wabunge mjini Kiev katika ziara iliyopangwa kuonyesha uungwaji mkono wa Marekani kwa serikali ya mpito ya Ukraine.
Bwana Biden amesema kuwa uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi ujao ni muhimu zaidi katika historia ya taifa hilo.
Wakati huohuo Biden amesema kuwa Marekani haitawai kutambua alichosema ni Udhibiti haramu wa jimbo la Crimea ambalo linadhibitiwa na Urusi.
Amesisitiza kuwa Ukraine ni nchi moja na inapaswa kusalia hivyo.
Amesihi Urusi,kuhakikisha kuwa mkataba uliofikiwa wiki jana wa kusitisha mgogoro kwa kuamuru vikosi vya Ukraine vinayounga mkono Urusi nchini humo kuondoka katika majengo ya serikali waliyoyateka Mashariki mwa Ukraine.chanzo BBC
0 comments :
Post a Comment