Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda ametoa ruksa kwa wanachama wanaounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) kufanya mikutano yao nchi nzima. Pinda
alizungumza jana wakati akifunga maonyesho ya miaka 50 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam, alisema yaliyotokea bungeni yanaweza kumalizika kwa kukaa meza
moja ya majadiliano.“Yale
mambo ya bungeni yanaweza kumalizika na tukaendelea kama ambavyo
ilikuwa katika majadiliano ya kutengeneza kanuni. Tulikuwa
tukishindana kwa kukaa meza moja na kumalizana, kisha tunaendelea sasa hili tumeshindwa nini?” alihoji Pinda Alisema:
“Walitoka bungeni na kusema watazunguka nchi nzima, nasema wazunguke tu
kuwaeleza wananchi na sisi hatutashindwa kuzunguka kwani hoja tunazo.”Waziri
Mkuu Pinda alitumia nafasi hiyo kuelezea kauli aliyoitoa Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kwenye
Kanisa la Methodist kwamba hoja ya serikali tatu ikipita inaweza
kulifanya jeshi kuchukua madaraka.Alisema nilimpigia simu nikamweleza: “Rudi mara moja ueleze kilichotokea huko na nafikiri mlimsikia alichokisema.”Lukuvi
akitoa ufafanuzi bungeni bila ya kuwapo kwa Ukawa alisema: “Nayasema
yote haya kwa kuwa naamini huo ndio msimamo wangu na utakuwa msimamo
ambao wakati wote utaendelea kuwa hivyo na ninawataka ndugu zangu kuacha
unafiki.”Kutokana
na kauli hizo, Ukawa inayoundwa na vyama vya Chadema, CUF, DP na
NCCR-Mageuzi na wajumbe 25 kutoka kundi la 201 walitoka bungeni Jumatano
wiki hii na kuahidi kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara
kuwaleza wananchi kilichotokea.chanzo mwananchi
SOURCE:MATUKIO NA VIJANA
0 comments :
Post a Comment