NAHODHA
wa Liverpool, Steven Gerrard ameanfgusha kilio cha furaha baada ya timu
yake kuukaribia ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza baada
ya miaka 24 kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidinya mahasimu wao katika
mbio za taji, Manchester City jioni hii Uwanja wa Anfield
Bao
la furaha la Liverpool limefungwa na Philippe Coutinho dakika 12 kabla
ya filimbi ya mwisho, baada ya mabao mengine ya timu hiyo kufungwa
kipindi cha kwanza na Raheem Sterling dakika ya sita na Martin Skrtel
dakika ya 26.
Lakini
City ilipigana na kusawazisha hadi kuwa 2-2 kwa mabao ya kipindi cha ya
David Silva dakika ya 75 na Glen Johnson aliyejifunga dakika ya 63,
lakini makosa ya Nahodha wa City, Vincent Kompany yalimpa Coutinho
nafasi ya kaumua mshindi wa mechi.
Baada
ya mechi, Nahodha wa Wekundu hao, Gerrard alionekana kumwaga machozi
kabla ya kuwakumbatia wachezaji wenzake. Liverpool sasa inatimiza pointi
77 baada ya kucheza mechi 34 na kuendelea kujinafasi kileleni, wakati
City inabaki na pointi zake 70 za mechi 32 na kuendelea kubaki nafasi ya
tatu. Chelsea yenye pointi 75 za mechi 34 ni ya pili.
Shujaa: Philippe Coutinho akishangilia baada ya kuifungia bao la ushindi Liverpool dhidi ya Manchester City leo
0 comments :
Post a Comment