Arsenal wakishangilia ushindi wao usiku huu.
WASHIKA
bunduki wa London, Arsenal FC wamezidi kujihakikishia kubaki Nne Bora
kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kuibamiza bao 3-0 Newcastle usiku
huu kwenye Uwanja wa Emirates jijini London.
Mabao ya Arsenal yamewekwa kimiani na Laurent Koscielny, Mesut Ozil and Olivier Giroud.
Kwa
matokeo ya leo, Arsenal wamefikisha pointi 73 baada ya kucheza mechi 36
wakiwa nafasi ya nne huku anayewafuatia kwa nyuma Everton akiwa na
pointi 69 baada ya mechi 36 wote wakibakiwa na mechi mbili mkononi.
0 comments :
Post a Comment