Timu ya
Taifa ya Tanzania, Taifa stars imechapwa mabao 3-0 dhidi ya Burundi
katika mechi ya kirafiki ya kuadhimisha miaka 50 ya muungano, uwanja wa
Taifa, jijini Dar es salaam.
Mmechi
hiyo imechezeshwa na refa Anthony Ogwayo kutoka Kenya akisaidiwa na
Gilbert Cheruiyot na Oliver Odhiambo wote pia kutoka Kenya.
Mwamuzi wa mezani alikuwa Israel Mujuni wa Tanzania wakati Kamishna ni Charles Ndagala.
Mabao ya Burundi yamefungwa na Didier Kavumbagu, Amis Twambwe wanaocheza soka la kulipwa nchini Tanzania.
Bao la
tatu la Burundi limefungwa na Yufuf Ndikumana na kuifanya Stars
iwahuzunishe watanzania waliokuwa na furaha ya kuadhimisha miaka 50 ya
muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
0 comments :
Post a Comment