Makala maalum kwa hisani ya (Salma Said)
Mwaka 1984, Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, na Makamo wa Pili wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Aboud
Jumbe Mwinyi, alilazimishwa kujiuzulu katika
Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma akishutumiwa
kutaka kuvunja Muungano. Kitendo hiki
kimekuwa kikichukuliwa na Wazanzibari kama
udhalilishaji mkubwa kwa nchi na heshima yao,
na msimamo wa serikali tatu, ambao Jumbe
anasemekana kuutetea umekuwa ndio
msimamo wa Wazanzibari. Kujiuzulu kwa Jumbe
kunaunganishwa na tafauti za kimtazamo baina
yake na Katibu Mkuu wa sasa wa CUF, Maalim
Seif Sharif Hamad, ambaye hata hivyo
anasisitiza katika makala hii kwamba hajawahi
kutafautiana na Jumbe kuhusu mtazamo wa
Muungano.
Kwanza niweke kumbukumbu sawa. Mwaka
1984 wakati Mzee Aboud Jumbe anajiuzulu
nyadhifa zake zote, mimi ni kweli nilikuwa
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mkuu wa
Idara ya Uchumi na Mipango ya Sekretarieti ya
Halmashauri Kuu ya Taifa [NEC] ya CCM, na
hivyo kuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa
Chama cha Mapinduzi. Hata hivyo wakati huo
sikuwa miongoni mwa viongozi wa Serikali ya
Mapinduzi. Kwani nilikuwa Waziri wa Elimu wa
Zanzibar kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka
1980. Nikateuliwa kuwa Waziri Kiongozi wa
Zanzibar na Mzee Ali Hassan Mwinyi
aliyeteuliwa kuwa Rais wa Muda wa Zanzibar
mara baada ya Mzee Aboud Jumbe kujiuzulu
mwaka 1984. Hivyo kuanzia mwishoni mwa
1980 hadi mwanzoni mwa 1984 sikuwa kiongozi
katika Serikali ya Mapinduzi.
Pili, tangu Chama cha Wananchi CUF kiasisiwe
hapo 1992, sera yake rasmi ni kuwepo kwa
Muungano wa serikali tatu: yaani Serikali ya
Muungano, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya
Tanganyika.
Pengine itakumbukwa kuwa hata Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema kuwa
Chama cha Siasa chochote kile kina haki ya
kuwa na sera yake juu ya Muungano. Akasema
kuwa kama vile ni haki ya CCM kuwa na sera ya
serikali mbili kuelekea serikali moja, CUF
wanayo haki hiyo hiyo ya kuwa na sera ya
serikali tatu katika Muungano. Mwalimu
Nyerere akamalizia kwa kusema kuwa na sera
juu Muungano inayotafautiana na sera ya CCM
si uhaini. Waachiwe wananchi waamue!
Hivyo basi msimamo wangu tangu kuasisiwa
kwa Chama cha Wananchi, CUF haujapata
kubadilika. Ni msimamo na sera ya Chama
changu cha CUF. Sera ya kuwepo kwa serikali
tatu katika Muungano wetu.
Hivyo niseme, kama nilivyokuwa nikisema kila
nilipopata nafasi, kuwa bila ya kuubadili
muundo wa Muungano wetu kutoka muundo wa
sasa wa serikali mbili kwenda kwenye muundo
wa serikali tatu, matatizo ya Muungano
yataendelea kuutafuna Muungano wetu. Badala
ya kuuimarisha tutakuwa tunaendelea
kuudhoofisha. Kuimarisha Muungano sio
kuongeza orodha ya Mambo ya Muungano
katika Katiba. Hili linadhoofisha Muungano.
Kwani nguvu za Muungano zitatokana na
wananchi wa pande mbili kuukubali kwa dhati
Muungano wenyewe. Kuhakikisha kuwa
wananchi wa pande zote mbili wanaridhika na
muundo wake, mamlaka na madaraka ya kila
upande na serikali yake. Na zaidi kuliko yote,
wananchi wa pande zote mbili kuridhika kuwa
wanatendewa haki katika Muungano.
Vyenginevyo tutakuwa tukibadili misamiati tu:
mara tutayaita matatizo ya Muungano; mara
tuziite kero za Muungano, pengine tutakuja
kuyaita mapungufu ya Muungano, au hata
bughdha za Muungano, na kadhalika.
Suala la kutoka serikali mbili kwenda serikali
moja hilo halitakubalika. Mimi silikubali. CUF
hailikubali, na Mzanzibari mzalendo yeyote
halikubali. Siamini kuwa Serikali ya Muungano
itakuwa tayari kutumia vifaru, mizinga na
madege ya kivita kulazimisha muundo wa
serikali moja.
Baada ya kuweka msimamo huo, sasa nigeukie
mambo mengine uliyoniuliza.
Kwamba Mzee Aboud Jumbe alituhumiwa
kutaka kuwepo kwa muundo wa Muungano wa
serikali tatu na akalazimishwa kujiuzulu. Wakati
huo mimi nilitetea muundo wa sasa wa serikali
mbili.
Ili hili lifahamike vyema na wananchi ni vyema
kwanza kuelezea mazingira yaliyomfikisha Mzee
Aboud Jumbe kujiuzulu.
Nitangulie kueleza kuwa mimi binafsi na kwa
dhati ya nafsi yangu namuheshimu na
namthamini sana Mzee Aboud Jumbe. Kwanza
ni mwalimu wangu nilipokuwa nasoma katika
skuli ambayo wakati huo ikiitwa The King
George VI Secondary School (sasa Lumumba
College).
Pili, ni Mzee Aboud Jumbe ambaye alisababisha
mimi kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
mara baada ya yeye kuwa Rais wa Zanzibar
mwaka 1972, baada ya kukaa kwa miaka
minane (8) tangu nilipomaliza masomo ya
Kidatu cha Sita (Form VI) hapo 1963 na kuzuiwa
na Serikali ya Mapinduzi kujiunga na masomo
ya Chuo Kikuu, pamoja na kuwa kila mwaka
nilikuwa napata nafasi katika vyuo mbali mbali
duniani.
Tatu ni Mzee Aboud Jumbe huyo huyo
aliyesababisha mimi kuwa kiongozi katika
Serikali ya Mapinduzi na kuwa miongoni mwa
viongozi wa juu wa CCM. Hivyo namshukuru na
katu siwezi kumsahau kwa mchango wake
mkubwa ulionifanya nilivyo.
Sasa nirejee kuelezea mazingira ya wakati huo
ambayo yalikuwa kama ifuatavyo:
Nianzie mwaka 1982 ambapo kulikuwa na
uchaguzi wa viongozi wa CCM. Katika kipindi
kilichotangulia Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM
wa 1982 wa kuchagua viongozi wa kitaifa,
kulijitokeza makundi mawili miongoni mwa
viongozi wa CCM kutoka Zanzibar yaliyokuwa
yakikinzana. Kundi la kwanza likijulikana kama
Liberators, na la pili likijulikana kama
Frontliners. Kundi la Liberators kimsingi
lilikuwa na viongozi ambao walikuwa wanapinga
mabadiliko ya aina yoyote yale katika
uendeshaji wa mambo ya kisiasa, kiuchumi na
kijamii katika Zanzibar.
Kwa lugha ya sasa unaweza ukaliita kundi la
Wahafidhina. Kundi la Frontliners lilikuwa na
vijana, damu mpya iliyoingia katika uongozi wa
Chama na SMZ. Kundi hili lilitaka mabadiliko
katika uendeshaji wa mambo ya kisiasa,
kiuchumi na kijamii. Unaweza ukaliita kundi la
Reformers.
Uchaguzi wa viongozi wa kitaifa (Wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa) wa 1982 ulishuhudia
msuguano mkali kati ya makundi hayo mawili.
Nia ya Liberators ilikuwa ni kuhakikisha kuwa
Frontliners hawaingii katika Halmashauri Kuu ya
Taifa. Nia ya Frontliners ilikuwa ni kuhakikisha
damu mpya inaingia katika kikao hicho kikuu
cha maamuzi cha Chama ambacho wakati huo
kilikuwa ndio kimeshika hatamu zote za uongozi
katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bahati njema Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM,
kwa busara zake, uliwaingiza watu kutoka
makundi yote mawili katika NEC na, baadaye,
NEC ikawaingiza watu kutoka makundi yote
mawili katika Kamati Kuu.. Frontliners
walishukuru kuona kuwa miongoni mwao
walifanikiwa kuchaguliwa kuingia katika vikao
vyote viwili vikuu vya maamuzi vya Chama.
Kwa upande mwengine, Liberators
hawakufurahi. Liberators hao walishaweka
shinikizo kwa Mzee Aboud Jumbe (ambaye
ndiye chanzo cha kuingiza damu mpya katika
CCM ya wakati huo) kuwa vijana aliowaingiza
watakujamgeukia na kuwaondoa wao,
Liberators, na yeye mwenyewe katika uongozi.
Inaelekea Mzee Aboud Jumbe alishawishika na
shinikizo hilo, na hivyo naye, kwa njia zake
(nyuma ya pazia), alitaka kuona kuwa
Frontliners hawaingii katika NEC na Kamati Kuu
ya Chama ambako pengine wangekuwa na
ushawishi katika maamuzi ya sera za Chama.
Frontliners walipoingia, ikawalazimu Liberators
na Mzee Aboud Jumbe kutafuta njia nyengine
ya kuweza kuwazingira ili, ikiwezekana, waweze
kuondolewa katika ramani ya uongozi wa
Chama na Serikali.
Hivyo basi, mara baada ya kikao cha Mkutano
Mkuu wa Taifa kumalizika mwezi Novemba,
1982, Mzee Aboud Jumbe aliwataka Wajumbe
wote wa NEC kutoka Unguja akutane nao
Unguja, na Wajumbe wote wa NEC kutoka
Pemba akutane nao Pemba. Katika mikutano
hiyo, hotuba ya mwalimu wangu, Mzee Aboud
Jumbe, ilitushtua wengi. Mzee Aboud Jumbe
alishtumu kuwa kuna watu wanaoleta uchochezi
kutaka kuvigawa visiwa vya Unguja na Pemba;
kutaka kuigawa mikoa, yaani mkoa mmoja dhidi
ya mwengine katika kila kisiwa; kutaka kuzigawa
wilaya, yaani wilaya moja dhidi ya nyengine
katika kila mkoa; na kutaka kuvigawa vijiji, yaani
kijiji kimoja dhidi ya chengine katika kila wilaya.
Akamalizia kwa kusema kuwa watu hao
watahukumiwa na kuonja kile alichokiita
“Revolutionary Justice”
Hili lilitushtua wengi, hasa sisi vijana wa wakati
huo. Tukakumbuka histor
BY NASHIR KAMUGISHA

0 comments :
Post a Comment