KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 7)
Kijana mmoja aliefahamika kwa jina la Kabi aliyekuwa akijituma kwa kufanya kazi mbali mbali ili amuwezeshe mdogo wake wa kike aweze kusoma ili aje kumsaidia baadae,Alituma pesa shilingi laki mbili kupitia tigo pesa kwa mdogo wake aliyekuwa anasoma shule ya sekondari Lugoba iliyopo mkoa wa Pwani ikiwa na ada pamoja na pesa ya kujikimu katika masomo na maisha ya shuleni hapo.Kwa bahati mbaya pesa ile ilienda kwa mtu mwingine ambaye hakumkusudia kabisa.Alipotiza kwa makini akakuta jina la mtu aliyepokea pesa si la mdogo wake bali ni jina la kiume ambalo lilikuwa geni machoni mwake.
Kijana mmoja aitwae Chambuso Kilitu alishangazwa kuona akaunti yake ikiwa imeingiziwa shilingi laki mbili na mtu asiyemfahamu.Haraka haraka akazima simu yake na kuanza kukimbia kwenye sehemu wanapotoa huduma ya tigo pesa.
Kijana Kabi baada ya kugundua tu kwamba amekosea kutuma pesa na kumrushia mtu mwingine akaanza kujuta na kufikiria wa jinsi zile pesa zilivyopatikana.Ghafla likamjia wazo kichwani na akaanza kucheka kisha akatoa simu mfukoni na kuanza kuandika meseji.ujumbe wake ulisomeka hivi
"UMECHAGULIWA KUWA MEMBER WA FREEMASONS HIVYO WEWE UTAKUWA WAKALLA WETU KATIKA NCHI YA TANZANIA.TUMEKUTUMIA SHILINGI LAKI MBILI KAMA KIAMBATANISHO CHAOMBI YETU YA WEWE KUWA WAKALA WETU.TAFADHALI USIMWAMBIE MTU YOYOTE KUHUSU SWALA HILI,BALI NENDA KATOE PESA HIYO KISHA RUDI NYUMBANI KIMYA KIMYA NA BAADA YA SIKU TATU MIHIMILI MITATU YA FAMILIA YAKO ITAKUFA KISHA UTATAKIWA ULALE NA MAITI HIZO KITANDA KIMOJA KWA SIKU TATU MFULULIZO KISHA UTAWAZIKA WAKIWA NA VIUNGO PUNGUFU.KWANI UTATAKIWA UBAKI NA MKONO WA KILA MMOJA WAO NA UTAHIFDHI MIKONO HIYO NDANI KWAKO MIAKA YOTE YA MAISHA YAKO PASINA WATU KUJUA.
TUNATUMAI UTAKUBALI OMBI LETU
NB:KAMA HAUTOKUBALI OMBI LETU BASI RUDISHA PESA HIZO PASINA KUMTAARIFU MTU YOYOTE."
Chambuso akiwa amekwishafika kwenye kibanda cha tigo pesa na kuwasalimia wadada wa kwenye kibanda hicho akaitoa simu mfukoni ili aweze kuzitoa pesa hizo kwa wakala kabla hazijachukuliwa na watu wa huduma kwa wateja,Simu ilipowaka tu mlio wa meseji ukaita katika simu ya Chambuso,Akataka asisome mpaka atakapotoa pesa ila akasema ni vyema nisome ujumbe huu huenda ukawa na maana.Ndipo alipokutana na ujumbe huo uliomtisha na kumfanya ageuze pasina kuaga kwenye kile kibanda.Akiwa njiani akasema siwezi kuwa freemason hata iweje ngoja nirejeshe pesa zao kabla sijamwambia mtu yoyote.Hivyo akarejesha pesa yote na kujisifu yeye ni shujaa kwa kuwagomea mualiko wao wa kuwa freemason.
Basi Kabi akapata pesa zake na kumtumia mdogo wake mpendwa
JE KAMA WEWE UNGEKUWA KABI UNGEFANYAJE???

0 comments :
Post a Comment