KISA CHENYE MAFUNZO (VOL 5)
Kijana mmoja alisomeshwa na baba yake mpka chuo kikuu,kisha akafanikiwa kupata kazi iliyomuingizia kipato kikubwa sana.Maisha yalikuwa mazuri kila kukicha huku umri nae ukienda,Alifanikiwa kupata watoto kadhaa ambao nao waliwapeleka shule sasa wamefanikiwa kufika elimu ya sekondari huku wakiwa na maendeleo mazuri katika masomo yao.
Yule kijana akawa anatembelewa sana marafiki zake ambao alisoma nao chuo kikuu pamoja na wafanyakazi wenzake.
Kipindi hicho chote alikuwa akiishi nyumba moja na yule baba yake ambae tayari alishakuwa mzee sana kiasi cha kumtegemea mwane kwa kila kitu.
Siku yule kijana akawaita watoto wake na kuwaambia kwamba amefikiria kwenda kutengeneza sanduku la kumuhifadhi baba yake kipindi wageni hasa marafiki zake wa chuo pamoja wafanyakazi wenzake watakapokuwa wanakuja nyumbani kumtembelea.Watoto wakamuuliza kwa nini unataka kumuhifadhi kwenye sanduku?Yule baba akasema kwamba anajiskia aibu sana kwa marafiki zake wanapokuja kumtembelea hasa yule babu yao akiwepo.....wale watoto wkamjibu je baba unapenda sana na sisi tusome mpka chuo?Yule baba akasema hiyo ndio ndoto yangu kwenu ntajitahidi kila liwezekanalo wanangu manfika chuo kikuu....wale watoto wakasema basi baba usitengeneze la mbao tengeneza la chuma ili na sisi tutakapopata kazi nzuri na wewe utakuwa mzee hivyo tutakuhifadhi humo ili rafiki zetu wasikuone usije kutuaibisha........Yule baba akainama chini kisha akasema kamwe sinto nunua sanduku humu ndani
HEBU TOA MAFUNZO ULIYOYAPATA KWENYE KISA HIKI
0 comments :
Post a Comment