-->

KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 4)MCHOYO ALIVYOKULA MIKOJO YAKE

 
KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 4)
Jamaa mmoja katika zama za zamani sana kabla ya ugunduzi wa magari,baiskeli meli na ndege alikuwa anasafiri jangwani kwa umbali mrefu sana huku akiwa na chakula cha kujikimu njiani.Alikuwa na tende ambazo ndio kilikuwa chakula pekee alichoweza kubeba kwa ajili ya msafara wake.
Alisafiri kwa muda mrefu pasina kufika kwenye safari yake,usiku ukaingia hivyo akaamua kutafuta sehemu ya kujihifadhi kwa kulala,akaiona nyumba moja maeneo ya karibu na alipokuwa hivyo akaamua kwenda kwenye nyumba hiyo na kugonga hodi.Alijibiwa na sauti ya kiume iliyojaa hekma na ukarimu,alimsalimia kabla ajaingia ndani na kuanza kueleza shida yake.Muungwana yule alimkubalia na kumruhusu kuingia ndanikuweza kujistiri kwa kulala..
Kulipokucha yule muungwana aliamua tikiti maji kubwa pamoja na sungura kama kotoweo katika msafara wake.Alipopewa vile vyakula na mwenyeji wake akamshukuru sana kisha akapata wazo kwamba kile chakula ni kingi sana hicyo akaona bora na yeye ampe zile tende kama zawadi.Kabla hajampa tende akapata wazo jingine kichwani mwake akimpa yule mwenye wake zile tende atafaidi sana kutokana na utamu wa zile tende.
Akaamua kuondoka na kuendelea na safari akiwa mizigo yake........Alisafiri umbali mrefu sana na kuanza kuona kwamba mizigo imekuwa mingi hivyo hanabudi kutupa mzigo mmoja.Akaamua kuzitupa tende....Kisha akaendelea na safari yake kbla hajafika mbali sana akapata wazo jipya kwamba pale alipozitupa tende kama akipita mpita nja basi ataziokota hivyo akaamua kurudi kisha akazinajisi kwa kuzikojolea na kuanza cheka kwamba sasa hapa mtu akiokota atakula mikojo yangu...
Baada ya hapo akendelea na safari na kufika mbali sana,akawa amechoka kutembea hivyo akaamua kujipumzisha chini ya mti mkubwa.Aliamua kumfunga yule sungura kwenye mti na tikiti kuliweka juu ya mti na yeye kuamua kulala chini ya mti.
Baada ya kupitiwa na lepe la usingizi,upepo mkali ulivuma na kudondosha tikiti kutoka juu na kamba ya sungura ilikatika hivyo sungura akakimbia.
Alipoamka hakuamini macho yake baada ya kukuta tikikiti likiwa limepondeka pondeka na kujaa michanga ya jangwani,alifikiria kusafiri bila chakula kuona ni vigumu kwani atakufa njaa.Akapata wazo la kurudi nyuma kuzifata tende zake alizozitupa,alirudi mpaka alipozitupa na kuzikuta kisha akakumbuka kwamba alizikojolea lakinia akajipa moyo kwmaba alikojelea pembeni kidogo na sio zote hivyo akaanza kuzila na kuendelea safari...........
HATIMAYE MCHOYO KALA MIKOJO YAKE...............................................
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment