-->

AJALI MBAYA YATOKEA,WATU 42 WAPOTEZA MAISHA

Tela la trekta likiondolewa eneo la ajali.
Ramani ikionyesha eneo ilipotekea ajali.
 WATU 42 wamepoteza maisha wakati 17 wakijeruhiwa baada ya basi la abiria lililokuwa likielekea Karachi nchini Pakistan kugongana na trekta lililokuwa na tela.
 Miongoni mwa waliopoteza maisha ni watoto 14 na wanawake 13. Ajali hiyo imetokea leo katika mji wa Sukkur, umbali wa kilomita 425 kutoka Karachi.
 Dereva wa basi amefariki papo hapo wakati wa trekta akijeruhiwa. Waliopoteza maisha wote walikuwa katika basi.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment