-->

UKAWA KUZUIWA KUFANYA MKUTANO WA HADHARA NI UOGA AU SHERIA???

UOGA AU SHERIA DHIDI YA.
UKAWA???
Katika hali inayoshangaza watu wengi ndani na nje, ni kupigwa maarufuku kwa UKAWA kufanya mkutano wao hapo kesho tarehe 19/04/2014 mjini Zanzibar
Hili kwangu limeniogopesha sana na kuona kuwa wana- Ukawa wamenyimwa haki ya kikatiba kama viongozi wa Vyama vyao. Katika jumuia yao kuna viongozi wa kitaifa kama Prof. Lipumba, Mbowe na Mbatia. Hawa ni viongozi ambao wanapaswa kuheshimiwa kama walivyo wale wa Serikali.
Lakini kitendo cha kuwanyima ruksa ya kufanya mkutano ni kuwavunjia nidhamu ya mamlaka yao katika taifa hili.
Mi na hofu kuona kuwa Tanzania tuitakayo haiwezi kupatikana bila katiba mpya yenye nchi mbili huru na zenye mamlaka kamili.
Si busara zilizotumika kuwanyima Viongozi hawa wasifanye mkutano huko Zanzibar. Hivi inaweza kuwa ni sababu za kiusalama au ni hofu tu ya kisiasa?
Tanzania ni nchi ya Vyama vingi na ya kidemokrasia Ibara ya 3(1), kama ni hivyo kwanini viongozi wa vyama na wengi ni waserikali kama Seif wanakataliwa kufanya mikutano? Hiyo demokrasi ipo wapi sasa? Au ni demokrasia kwa baadhi ya watu fulani? Mbona haijawahi kutokea kiongozi wa CCM anakataliwa kufanya mkutano kwa sababu za kiusalama?
Ndugu zangu hii nchi ni yakwetu sote, hakuna mwenye haki kuliko mwingine kama kweli ni kidemokrasia, ila kama ni ya Kidikteta. Hatuwezi kupongeza dhuluma ifanyike nasi tushangilie, hata kidogo, kama mtapiga makofi mimi niko radhi kubaki mwenyewe ni kilia na kuomba haki itendeke.
CCM naipenda sana kwa kuwa nafahamu misingi yake ilivyo, na hapo ndipo nikoradhi kuitetea popote pale kwa mazuri yake. Lakini ni budi sana kukosoa pale panapoonekana hapaendi sawa ima kwa kusababishwa na mwanachama, kiongozi au mtawala fulani.
Nilipenda sana kauli ya Katibu mkuu wa CCM ndg. Comrade Kinana aliyoitoa jana akiwa Katavi kuwa '' Milango iko wazi kuikosoa CCM na Viongozi wake kwa kuwa ndiyo demokrasia''
Hii kauli ni nzuri kwa wenye busara tu, na wale makanjanja wataiona haifai kwa kuwa hawataki kukosolewa kwa matendo mabaya wanayofanya katika kudidimiza taifa hili. Mfano mzuri ni ile kauli ya Lukuvi aliyoitoa Kanisani kuwa Zanzibar ikijitenga itaongozwa katika mfumo wa kiislamu. Hii ni kauli ya kichochezi, kiubaguzi na inaonyesha chuki yake dhidi ya Waislamu.
Kwa hili namshauri kwa niaba ya serikali ajiudhuru ili kuiachia Nchi ipumue sivyo itasababisha mambo yaliyofichwa yatolewe.
Kila Nchi inasiri nyingi za kiutawala lakini kwa TZ itakuwa imefikia mwisho katika utunzaji wa siri hizi. Na hii imesababishwa na watu kama Lukuvi kuanza kutugawa kidini, kiukanda na kimakabila.
Naomba tena, utu uzima wake autumie kujiudhuru ili kupisha Rais kuteua mtu mwingine mwenye busara kuongoza Sera na Uratibu wa bunge, maana busara zake zimefika mwisho.
Nchi hii imevimba inapaswa kupumua sasa na ikicheleweshwa itapasuka yenyewe, hapo itakuwa haiwezekani tena kurudishwa katika amani iliyodumu kwa miaka zaidi ya 50. Viongozi wa Chama changu cha Mapinduzi, tuangalie na tuendane na madiliko ya Elimu, Technolojia, utandawazi na Demokrasia la sivyo tutaipeleka Nchi katika machafuko makubwa na yatakayotugharimu sana mali zetu, uhuru wetu, amani yetu na umoja wetu.
Mungu ibariki Tanganyika, Zanzibar na Jamuhuri ya Tanzania . Amin
BY TWALLYIB YASSINI
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment