-->

KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 8)WAHUJUMU WA NCHI

KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 8)
Hapo zamani kulikuwa na nchi mbili moja ikifahamika kwa jina la Uganzo na nyingine ikifahamika kwa jina la Nzotani.Siku moja wazili wa mambo ya ujenzi wa Nzotani aliamua kumtembelea wazili wa wa ujenzi wa nchi ya Uganzo.Alipofika nchini Uganzo alishangazwa sana na jumba kubwa la wazili wa nchi hiyo ya Uganzo hivyo ikabidi amuulize
Mwenzangu ulifanikiwaje kupata pesa ya kujenga mjengo huu,Wazili wa uganzo akajibu kwamba ili ufahamu hayo twende lotion ya juu ya nyumba yangu.Walipofika juu wakawa wanaiona nchi ya Uganzo kwa uzuri kabisa hivyo akaanza kumwambia unaliona daraja lilee,Wazili wa Nzotani akatizama kwa umakini na kuliona daraja hilo lililokuwa mbali na pale walipo.Basi chenchi ya daraja lile ndio nyumba hii.
>>>>>>>>>>>>>Miaka kadhaa ikapita<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
Wazili wa Uganzo nae akaenda Nzotani alipofika huko Nzotani akakaribishwa kwenye jumba la kifahari la wazili wa mambo ya ujenzi.Alishtuka na kushangazwa zaidi na kuladhimu aulize ndugu yangu uliwezaje kujenga jumba la kifahari kama hili??
Wazili wa Nzotani akajibu,ili kufahamu hayo twende ghorofa ya n ya mwisho ya nyumba yangu.
Walipofika juu kabisa wazili wa Nzotani akaanza kumwambia unaliona lile daraja kulee.....??Wazili wa ujenzi wa Uganzo kila akitazama haoni kitu kiasi cha kushangazwa na kauli ya wazili wa Nzotani,hivyo akahoji busara iliyonyuma ya kauli ya wazili wa Nzotani.....kisha wazili wa Nzotani akajibu kwamba pesa yote ya daraja ambalo lilitakiwa kujengwa pale ndio nimetumia kujenga nyumba hii...........
JE UMEJIFUNZA NINI KUTOKANA NA KISA HIKI????
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment