-->

DONDOO ZA AFYA:USHAURI WA LISHE NA ULAJI KWA MTU MWENYE UGONJWA WA FIGO



Magonjwa ya figo
Figo hufanya kazi muhimu mwilini ambazo ni:-
• Kudhibiti na kuhifadhi virutubishi na maji na kuondoa mabaki kupitia mkojo.
• Kuchuja damu ili kuondoa mabaki ambayo ni sumu mwilini. Baadhi ya mabaki hayo ni urea, uric acid, creatinine na ammonia.
• Kudhibiti viwango vya electrolyte mwilini, yaani Sodium (Na+ ) na
Potassium (K+). Sodium husaidia kudhibiti wingi wa maji mwilini na pia huwezesha mawasiliano kati ya mfumo wa fahamu na misuli (enhances
commucacation between brain/nerves and muscles). Potassium husaidia mapigo ya moyo between brain/nerves and muscles). Potassimu husaidia
mapigo ya moyo (regulates heart beats) na kazi ya misuli (muscle function). Viwango vya kawaida kwa Sodium ni 135-145 mmol/L na
Potassimu ni 3.5-5 mmol/L.
• Kudhibiti shinikizo la damu kupitia mfumo wa rennin-angiotension.
• Kutengeneza kichocheo cha Erythropoietin ambacho huchochea utengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu.
• Kuchochea vitamin D ambayo hutumika katika kudhibiti kiwango cha Calcium na Phosphorous kwenye mifupa.
Iwapo mtu atapata ugonjwa wa figo ambao utaathiri figo zote mbili, kazi zote hizo hapo juu huathirika au kushindwa kufanyika kwa ufanisi na
madhara hutokea kutengemea kiwango cha athari. Figo zinaweza kushindwa kufanya kazi aidha kwa sababu za kipindi kifupi (acute renal
failure) au kwa sababu za muda mrefu (chronic renal failure).
Sababu zinazoweza kufanya figo zishindwe kufanya kazi:
i) Katika muda mfupi:
o Upungufu mkubwa wa ujazo wa damu (kupoteza damu kwa kiasi kikubwa)
o Upungufu wa maji mwilini kutokana na kutapika, kuhara, na homa
o Matumizi ya baadhi ya dawa kama diuretics
o Mawe kwenye figo (kidney stones)
o Maambukizi kwenye figo mfano sepsis
o Uvimbe –uchungu (inflammation) kwenye mfumo wa uchujaji kwenye figo (acute glomerulonephritis)
o Uvimbe mkubwa wa tezi dume (prostatic hypertrophy)
o Saratani ya tezi dume (prostate cancer)
ii) Katika muda mrefu
o Kisukari kisichodhibitiwa
o Shinikizo kubwa la damu lisilodhibitiwa
o Uvimbe-uchungu wa kudumu kwenye mfumo wa uchujaji wa figo(chronic glomerulonephritis)
o Mawe kwenye figo
o Magonjwa ya tezi dume (Prostate disease)
Dalili za ugonjwa wa figo:-
Mwanzoni, ugonjwa wa figo hauoneshi dalili yeyote. Mara utendaji kazi wa figo unapopungua, dalili hujitokeza kuendana na udhaifu wa kudhibiti maji
na electrolyte mwilini; kuondoa mabaki mwili; kutengeneza erythropoietin ambayo huchochea utengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu,
na pia udhaifu wa kuchochea Vitamini D ambayo ni muhimu katika kuweka viwango sahihi vya calcium-phosphorous kwenye mifupa, misuli na neva.
• Dalili za mwanzo ni kama:-
o Kudhoofika,
o Kuchoka mara kwa mara
o Kukosa nguvu,
o Kukosa pumzi/kupumua kwa shida
o Kuvimba mwili (hasa usoni), na
o Homa isiyokuwa kali
Hali hii isipogundulika mapema huweza kusababisha hatari ya kupoteza maisha.
• Udhaifu wa kutoa Sodium (Na+) mwilini husababisha wingi wa Sodium mwilini (hypernatremia) ambao huambatana na kujaa kwa maji mwilini
(generalized oedema) kuongonzeka uzito ghafla, ongezeko la shinikizo la damu, kushindwa kupumua mwisho husababisha ugonjwa wa moyo (congestive heart failure).
• Udhaifu wa Potassium (K+) mwilini husababisha wingi wa potassium mwilini (hyperkalemia) ambao husababisha misuli kukosa nguvu au kuwa
dhaifu na mapigo ya moyo kuenda ovyo ovyo (arrhythmias) na ikizidi huweza kusababisha kifo cha ghafla.
• Kushindwa kutolewa kwa urea mwilini husababisha uharibifu kwenye ubongo (encephalopathy).
• Udhaifu kwa ujumla husababishwa na upungufu mkubwa wa damu ambao husababishwa na kushuka kwa uwezo wa figo kutengeneza erythropoietin hivyo chembechembe nyekundu za damu kupungua.
• Kukosekana kwa uwiano unaotakiwa kati ya phosphorous na calcium huweza kufanya mifupa kuwa miepesi kuvunjika.
Ushauri wa lishe na ulaji kwa mtu mwenye ugonjwa wa figo
Ulaji wa mtu mwenye ugonjwa wa figo unapaswa kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwani figo haziwezi tena kutoa mabaki ya protin, maji, chumvi na
potassium kwa urahisi inapozidi mwilini. Vyakula vyenye chumvi na potassium nyingi viepukwe ikiwa ni pamoja na kuzingatia mambo yafuatayo:
Mambo ya kuzingatia katika ulaji:-
• Punguza kiasi cha nishati-lishe. Kiasi cha nishati-lishe na protini kinapozidi mwilini huzipatia figo ambazo zimeathirika kazi kubwa.
• Punguza kiasi cha vinywaji/vimiminika- ili kupunguza kujaa kwa maji mwilini ambako husababishwa na kushindwa kwa figo kutoa maji mwilini.
Maji yakizidi mwilini husababisha kushindwa kupumua, shinikizo kuwa la damu, kuvimba mwili na huweza kusababisha
ugonjwa wa moyo (heart failure). Dhibiti ongezeko la uzito wa mwili kwani huweza kuonesha kuwa maji yamezidi mwilini.
• Punguza kiasi cha sodium: Kiasi cha maji mwilini hudhibitiwa na sodium. Pale sodium inapozidi mwilini husababisha maji kubaki mwilini. Hali hii huweza kusababisha ongezeko la uzito ghafla, kuvimba kwa viungio vya
mwili, shinikizo kubwa la damu, kushindwa kupumua na huweza kusababisha ugonjwa wa moyo. Vyakula vyenye sodium kwa wingi ni vyakula vilivyosindikiwa kwa chumvi (nyama, samaki, soseji, bacon). Jenga tabia ya kutoongeza chumvi kwenye chakula wakati wa kula.
• Punguza kiasi cha potassium: Madini ya potassium yanapozidi mwilini husababisha misuli kuwa dhaifu na mapigo ya moyo kubadilika na yakizidi
sana hueza kusababisha kifo cha ghafla. Ni muhimu kudhibiti kiasi cha potassium kwa ukaribu. Vyakula vyenye potassium kwa kiasi kikubwa ni
pamoja na maparachichi, ndizi mbivu, maboga, machungwa, pichesi, peasi, matunda yaliyokaushwa na maharagwe. Vyakula vyenye potassium kwa kiasi kidogo ni pamoja na zabibu, machenza, mahindi mabichi, cauliflower, na matango.
Unaweza kupunguza kiasi cha potassium kwenye chakula kwa kuchemsha na kumwaga maji za ziada.
Kiasi cha potassium kinachoshauriwa kwa siku kwa mtu wa kawaida ni gramu 4.7 (milligram 4,700). Kwa mgonjwa wa figo inashauriwa gramu 1.5-2.7 (milligram 1500-2700) kwa siku na kila mlo asizidishe gramu 0.25 (miligramu 250).
• Punguza kiasi cha phosphorus
Uwiano wa calcium na phosphorus mwilini ni muhimu kuwezesha afya njema ya mifupa, misuli na neva. Phosphorus inapozidi mwilini mifupa
huwa myepesi kuvunjika (brittle) na rahisi kuvunjika. Hii inatokana na mwili kutoa calcium kwenye mifupa vyakula ambavyo vina phosphorus kwa wingi
ni pamoja na maziwa na mazao yake, nyama, shellfish, vyakula amvavyo havijakobolewa, maharage, karanga, korosho na chokoleti.
Vitamini na madini ya nyongeza
Wagonjwa wa figo huhitaji vitamin na madini ya nyongeza kutokana na kutokula aina mbalimbali za vyakula na hivyo kuweza kusababisha
upunfugu wa baadhi ya virutubishi. Damu inapochujwa (dialysis) pia huondoa vitamin kwenye damu. Virutubishi vya nyongeza vitolewe kwa mgonjwa wa figo kwa ushauri wa daktari.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment