Baba mmoja aliyekuwa anaishi ameneo ya kanda ya ziwa alikuwa amejenga nyumba yake maeneo ya karibu na ziwa.Hivyo kutokana na mazingira kuwa mazuri zaidi kwa kilimo aliamua kulima ndizi kwa kupanda migomba mingi sana karibu sana na nyumba yake.baada ya maiezi kadhaa kupita migomba ilistawi na kuzaa ndizi nyingi sana zilizotengeneza kichaka chenye mithili ya msitu.Kwa kuwa mazingira hayo pia kulikuwa na nyumba nyingine za watu hivyo baadhi ya vyo majirani vilikuwa karibu na migomba yake.
Ndizi zilipokomaa wakajitokeza vibaka waliokuwa wakiiba mikungu ya ndizi hizo mara kwa mara huku mpandaji akimbulia majani ya migomba ya ndizi katiaka bustani yake ya migomba.
Akaamua kununua mshale ili aweze kulinda migomba hiyo mida ya usiku.Alijiapiza kumshughulikia mwizi atakayempata akiiba ndizi zake.
Akawa usiku anakesha nje ya nyumba yake akilitazama shamba lake kwa umakini sana.Wezi walishamshtukia hivyo wakaacha kuja.Siku moja akiwa nje akilinda shamba lake la migomba alipitiwa na usingizi na aliposhtuka tu akamuona mtu anatokea kwenye migomba,pasina kufanya ajizi alirusha mshale na kumpata kijana mmoja mdogo sana kiumri.Alimsogelea karibu ili amuongeze na upanga wa kichwa lakini alishindwa kufanya hivyo baada ya kugundua kuwa alikuwa ni mtoto wa jirani akitokea chooni kujisaidia huku pembeni kukiwa na kopo la uwani likiwa limeanguka chini na maji kumwagika.
Yule mzee alichanganyikiwa na kuamua kumuamsha mkewe,mkewe alishtuka sana na cjui wafanyaje.Akaamua kutoka kwenda kwa rafiki yake wa karibu aliyefahamika kwa jina la Maja,alifanikiwa kumkuta na kumuhadithia hali ilivyo.Akamwambia kama ameshakufa basi tumzike usiku huu huu kabla hapaja pambazuka....Akakubali ushauri wa rafiki yake hivyo wakamzika usiku ule wakiwa watu wa watatu kisha wakarejea nyumbni kabla usku haujaisha.
Baada ya masiku kadhaa kupita huku majirani wakiendeleza jitihada za kumtafuta kijana wao Maja alimtafuta rafiki yake na kumuomba kuteta nae jambo.Walipokuwa faragha akamwambia inabidi tumfukue yule kijana na kumzika sehemu tofauti na ile...Alishtuka na kugoma hoja hiyo lakini Maja hakusita kumshawishi mpka alipokubali.Basi usiku mmoja jamaa yule alimtoroka mkewe kwa siri na kwenda kuifukua maiti ile kisha kwenda kuizika sehemu nyingine na kutafuta mzoga wa mbwa na kuufukia kwenye lile kaburi la awali.
Baada ya hapo ilichkua maika mitatu pasina mtoto kupataikana na ndugu wakaeka matanga huku wengine wakiamini ya kwamba mtoto wao amefariki ingawaje hawakumuona,huku wengine wakiamini kwamba amechukuliwa na majini ya ziwani.
Siku moja yule bwana aliyeua alichukizwa na mkewe hivyo kuamua kumchapa makofi mawili matatu,cha ajabu yule mwanamke alitoka nje huku akilia kwa nguvu na kuita majirani wote waje nje kwani anasri ambayo leo anataka kuwaambia.Watu wote wakatoka nje na kuuliza kulikoni...jamaa akajitahidi kummnya kwa macho ili asiseme ile siri yao lakini mwanamke yule alipaniiki na kusema ni huyu MUUAJI,ANATAKA KUNIUA KAMA ALIVYOMUUA MWANENU.........watu walishtuka na kupiga simu polisi,pOLISI WALIPOFIKA WALIMCHUKUA MWANAMKE HUYO PAMOJA NA YULE KIJANA ILI WAKAONYESHE KABURI LA KIJANA HUYO........
Kwa bahati mbaya kwa yule mwanamke hakufahamu kama maiti ilishahamishwa kwenye kaburi lile....Hivyo aliwaonyesha polisi kaburi huku akiwa na confidence kabisa kwamba HUYU MUUAJI ALIMZIKA HAPA MTOTO WENU.....jambo la kushangaza walikuta maiti ya mbwa iliyokuwa ishajiozea vya kutosha...KUtokana na kutokuwepo kwa ushahidi mwanmke huyo aliendlea kushikiliwa na polisi mpaka aonyeshe wapi maiti ilipo huku jamaa akiendelea kuishi uraini
*********MWISHO**********
0 comments :
Post a Comment