-->

JE UNAJUA KWA NINI IVO MAPUNDA HUTUMIA TAULO GOLINI?BOFYA HAPA KUFAHAMU


                                Ivo Mapunda akiwa Gor mahia nchini Kenya
Ivo Mapunda golikipa wa timu ya Simba kitika mchezo dhidi ya Yanga fc alining'iniza taulo kwenye goli lake kitu ambacho kimetafsiliwa na mashabiki wengi wa Yanga pamoja na wachezaji wa Yanga kama ni taulo la kishirikina ambalo lilikuwa linachangia kuwanyima magoli.
Ivo Mapunda amekuwa akininginiza taulo golini katika maisha yake yote ya golini,akiwa nchini Tanzania na hata nchini Kenya.Kama taulo hilo lingekuwa na dawa ya kuzuia magoli basi  Simba angekuwa bingwa wa VODACOM PREMIER LEAGUE kwani asingefungwa mechi hata moja.Ktika mchezo dhidi ya Ashanti fc timu ya Simba walifungwa moja na taulo ya Ivo Mapunda ikining'inia kwenye nyavu za goli.
Tukio hili la watu kutilia shaka taulo la Ivo Mapunda sio la kwanza kwani alipokuwa nchini Kenya katika mechi ya fainali kati ya Gor mahia dhidi ya Sofapaka,Ivo Mapunda alikuwa akitumia taulo hiyo kujufuta kila baada ya kucheza penati tendo ambalo lilimfanya George Owino kwenda kulitoa taulo hilo na kuanza kusambaa kwa tetesi kwamba n taulo la kichawi(black magic).
JE IVO MAPUNDA ANAZUNGUMZIAJE SWALA HILO??
“There was nothing in the towel, I normally carry it (towel) during all my games, and use it to wipe dirt and sweat during matches. I cannot allow it to be on the ground because it will get dirty,” Mapunda told Goal.com.
Akimaanisha kwamba hutumia taulo hiyo kwa ajili ya kujifutia uchafu,pamoja na jasho wakati wa mechi.Pia anasema hawezi kuliweka chini kwa sababu anahofia kuchafuka
JE SHERIA ZA SOKA ZINASENAJE KUHUSU HILO
“The law is quite silent on that. Law one of the FIFA rules however state that, in the field of play, the goalpost shall be fixed with a goal net which should not carry anything on it. If we have to go by the law, then the towel should be nowhere near the keeper’s goal area. But this is quite contentious because the law is quite silent on the use of a towel by a keeper,” Kenyan Top referee Nasur Doka told michezoafrika.com.
Kwa kauli ya jumala inaonekana kwa mujibu wa sheria za FIFA  hairuhusiwi kwa golkipa kuweka kitu chochote golini lakini hiyo pia haikuzungumza kitu kuhusu matumizi ya taulo.
JE IVO MAPUNDA NDIO GOLOKIPA PEKEE ANAYETU MIA TAULO??
Hapana magolikipa wengi sana wa Ulaya hutumia taulo.Wengine huyaweka ndani ya nyavu na wengine huyaning'iniza kwenye nyavu
Tim Howard golikipa wa timu ya Everton akiwa na
 taulo yake ikining'inia kwenye nyavu ya goli.Pia golikipa wa Manchester united Lindergaad alining'niza taulo katika mechi ya Newcastel mwaka 2012
kwa taarifa zidi kuhusu Ivo na taulo
                                           >>>>>>>>>>>>>soma zaidi<<<<<<<<<<<<<<
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment