-->

KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 12)JINSI EMBE LILIVYO MKUMBUSHA KIJANA KUHUSU UKUBWA WA MUNGU

KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 12)
Kijana mmoja ambaye alikuwa na imani yenye kutetereka,Baada ya uchovu wa kazi nyingi za kidunia akaamua kutafuta sehemu ya Alikwenda kukaa karibu na mti wa muembe ili apate kivuli cha mti huo.
Alopochoka kusimama chini ya mti akaamua kukaa chini kabisa,Alipokaa chini akaona maboga pamoja na matikiti yaliyokuwa yamepandwa karibu na mti huo.
Akaanza kulaumu na kumshtumu Mungu kwamba hakufanya uamuzi sahihi kwa kuweka matunda muhim kama tikiti chini ya ardhi baadala ya kuweka chini matunda ya kawaida kama vile maembe sindano.
Muda mchache baada ya kujipumzisha chini ya mti huo embe moja likadondoka kutoka juu ya mti na kutua kichwani kwake.Alihisi maumivu makali sana kuchwani kwa kupigwa na embe hilo kisha akajiuliza kama embe ndogo kama hii imenisababishia maumivu makali kiasi hiki vipi matikiti yangekuwa yanakaa juu.Kutoka hapo aliheshimu sana maamuzi ya Mungu katika uumbaji na mpangilio vitu na viumbe.
FUNZO:Kila kiumbe unachokiona jinsi kilivyo na mahala kilpo,tambua nyuma yake na kuna busara na hekama na Mola ambaye ni muumbaji wa mbingu na ardhi.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment