Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
HATIMAYE
safari ya mechi 26 za ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014
imemalizika leo kwa timu zote 14 kushuka uwanjani katika miji tofauti
nchini.
Yanga
waliovuliwa ubingwa na Azam fc walikuwa wenyeji wa watani zao wa jadi,
wekundu wa Msimbazi Simba sc kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Mechi
hii ya kulinda heshima kwa timu zote ilianza kwa timu zote kucheza kwa
umakini, lakini Simba walionekana kutawala mchezo huo na kufanya
mashambulizi mengi langoni mwa Yanga.
Katika
kipindi hicho cha kwanza, Amiss Tambwe, Said Ndemla kwa nyakati tofauti
walipata nafasi nzuri za kufunga lakini kukosa umakini kuliwanyima
Simba mabao.
Yanga
nao walifika mara kadhaa langoni mwa Simba, lakini Mrisho Ngassa na
Didier Kavumbagu walishindwa kuzibadili nafasi hizo kuwa mabao.
Kwa
ujumla kipindi cha kwanza kilikuwa katika himaya ya Simba kwasababu
walifika mara nyingi zaidi langoni mwa Yanga na pengine katika mechi za
nyuma wangekuwa wanacheza mpira kama ule wasingekuwa hapo walipo.
Kipindi cha kwanza kilimazika kwa timu hizo kutofungana.
Kipindi cha pili, Yanga walitawala zaidi mchezo, lakini dakika 75 Haruna Chanongo aliifungia Simba bao la kuongoza.
Dakika ya 86 ya kipindi hicho, Saimon Msuva alichomoa bao hilo na mechi kumalizika kwa sare ya 1-1.
Hata hivyo katika mchezo huo kulitokea vituko kadhaa.
Cha
kwanza ni mshambuliaji wa Yanga Didier Kavumbagu kutoa taulo la mlinda
mlango wa Simba Ivo Mapunda alilolitundika kwenye nyavu golini.
Kitendo hicho kinatafsiriwa kuwa ni imani za kishirikina kwa wachezaji wa Yanga walioamii taulo hilo limezuia mabao.
Kutokana na purukushani hiyo, mwamuzi wa mchezo huo alimzawadia kadi ya njano Kavumbagu na Ivo akapewa taulo lingine.
Dakika
chache baadaye, shabiki mmoja aliingia uwanjani na kuiba taulo la Ivo
na kulirusha kwa mashabiki wa Yanga, lakini alitiwa mbaroni na Polisi
walioshindwa kumuona wakati anaingia.
Hata
hivyo baada ya Simba kufunga bao, dakika chache baadaye, kocha msaidizi
wa Simba, Suleiman Matola na kocha wa makipa Idd Pazzi walitolewa ka
kadi nyekundu.
Kwa matokeo ya mechi zote endelea kutufuatilia na muda si mrefu utapata pamoja na uchambuzi
0 comments :
Post a Comment