KISA CHENYE MAFUNZO(PART 2)
Siku moja wanayasansi walikuwa wakibishana wengine wakisema MUNGU yupo na wengine wakisema MUNGU hayupo.
Waliosema Mungu hayupo waliulizwa swali kama MUNGU hayupo je dunia iliumbwa na nani?
Wakasema DUNIA ilitokea by chance(yaani ilitokea tu) pasina kuwa na muumbaji.Wengi waliamini katika hilo kwamba dunia ilitokea by chance,Mwanasayansi mmoja ambaye alikuwa bado anaamini MUNGU yupo aliamua kuwafanyia jambo flani wenzake.
Siku moja kabla ya kikao chao cha mambo ya kisayansi aliingia kwenye chumba cha mkutano kwa siri na kuamua kuweka mpira kwenye meza kisha akatoka.
Muda wa kikao ulipofika wanasayansi wote waliingia humo ndani na kuanza kujadili mambo mbali mbali ya kisayansi,kisha wakati walipomaliza kikao kila mtu alikusanya mafaili yake na kutaka kuondoka...Yule mwanasayansi akachokoza kwa kuuliza mpira huu ni wa nani??kila mtu akasema sijui...jamaa akasema inamaana hauna mwenyewe??wote wakanyamaza kimya kuashiria kutomfahamu mmiliki wa mpira ule.....
AKAWAAMBIA BASI MPIRA HUU UTAKUWA UMETOKEA BY CHANCE
wote wakabisha na kusema haiwezekani mpira utokee by chance kwenye chumba mikutano,walibisha kwa kiwango kikubwa sana...
Kisha akawaambia kama mpira mdogo hivi hamuamini kutokea kwake BY CHANCE vipi kuhusu dunia ambayo ni kubwa zaidi????
BASI WANAYANSI WENGI WAKAKUBALI KUWA MUNGU YUPO KASORO WACHACHE AMBAO WALIDUMISHA MISIMAMO YAO......
je umejifunza nini kwenye kisa hiki???????????????
0 comments :
Post a Comment