-->

WACHEZAJI WA BARCELONA WATOA HESHIMA ZAO ZA MWISHO KWA ALIYEKUWA KOCHA WAO TITO VILANOVA

395632_heroa
WACHEZAJI wa Barcelona wametembelea eneo maalum lililoandaliwa na klabu kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Tito Vilanova aliyefariki jana ijumaa. Vilanova aliyekuwa kocha msaidizi wa Pep Guardiola kabla ya kuwa kocha mkuu amefariki akiwa na miaka 45 kutokana na maradhi ya saratani ya koo. Baada ya kurithi mikoba ya Guardiola msimu wa 2012/2013, Vilanova aliiongoza Barcelona kutwaa ubingwa wa La Liga kwa pointi 100 na kuweka rekodi. Hata hivyo kazi yake nzuri iliingiliwa na maradhi na kulazimika kujiuzulu mwezi julai mwaka jana. Klabu ilithibitsha jana kuwa Vilanova amefariki na leo hii wachezaji na makocha wakiwa wageni wa kwanza, wametembelea eneo maalum liliotengwa kwa shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa Tito.
Tragic: Victor Valdes, Xavi and Carles Puyol are visibly upset as they pay tribute to Tito Vilanova
Tragic: Victor Valdes, Xavi and Carles Puyol are visibly upset as they pay tribute to Tito Vilanova

Sudden: Barcelona's former boss passed away on Friday after losing a battle with throat cancer
Sudden: Barcelona's former boss passed away on Friday after losing a battle with throat cancer

Dedication: Members of staff, including Tata Martino conducted a moments silence for Vilanova
Dedication: Members of staff, including Tata Martino conducted a moments silence for Vilanova


Twitter


Kocha mkuu Gerardo Martino akiwa na mkurugenzi mkuu Andoni Zubizarreta na rais Joesp Maria Bartomeu waliiongoza klabu kutoa salamu za rambirambi. “Baada ya kusaini kitabu cha rambirambi, kikosi kizima kilienda kuitazama picha kubwa ya Tito Vilanova, ambapo walikaa kimya kwa muda kama sehemu ya kutoa heshima kwake”. Barca wameandika kwenye Tovuti ya klabu. “Ilikuwa hali ngumu sana kwa wachezaji kumuona kocha wao aliyewafundisha wengi wao katika soka la ujana na akiwa msaidizi wa Pep na baadaye kuwa kocha mkuu”. Nahodha Carles Puyol alisema: “Kutoka hapa tunatuma salamu za pole kwa familia na marafiki”. Milango ya eneo hilo katika uwanja wa Camp Nou imeshafungulia kwa watu wote kwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa Tito
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment