Prof Paramagamba Kabudi ,atoa ya moyoni kuhusu Katiba,
Atumia weledi wake katika mambo ya kisheria kuuelezea Muungano.
Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Profesa
Palamagamba Kabudi amejibu
baadhi ya hoja za watu
wanaopendekeza muundo wa
serikali mbili na kusema Serikali ya
Zanzibar ndiyo iliyoanza kutaka
serikali tatu mwaka 1984.”
Aidha, amewashangaa wanaolibeza
jina la Tanganyika kutumika
serikalini kwa madai kuwa jina hilo
siyo haramu kwa kuwa limo ndani
ya Katiba ya sasa.
Alisema kuwa wakati huo madai ya
serikali tatu yalitolewa na Zanzibar
na kusimamiwa na Rais aliyekuwa
pia Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Alhaji Aboud Jumbe.
“Hoja ilipelekwa pia kwenye Baraza
la Wawakilishi, Brigedia Mstaafu
Ramadhan Haji Fakhi (aliyekuwa
Waziri Kiongozi), alikuwa akiongea
kwa sauti nzito, kama ulikuwa
ukimsikiliza, unasema muungano
haupo,” alisema Profesa Kabudi na
kueleza kuwa Fakhi alisema:
“Zanzibar siyo koloni la
Tanganyika.”
Alikuwa akichangia hotuba katika
Kongamano la Kujadili Miaka 50 ya
Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar, lililofanyika mjini
Zanzibar jana. Alieleza kwamba
mjadala wa sasa wa muungano siyo
mkali kama uliokuwepo mwaka 1983
na 1984.
Hata hivyo, hotuba hiyo ya Profesa
Kabudi iliyokuwa ikirushwa moja
kwa moja na Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC1) ilikatishwa kabla
mzungumzaji kumaliza hotuba yake.
Katika maelezo yake, Profesa
Kabudi ambaye pia ni Mhadhiri wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
alisema kuwa Fakhi alikuwa haongei
kama mtu baki, bali aliagizwa na
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
“Lugha ilikuwa ni kali,” alisema.
Akifungua kongamano hilo, Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib
Bilal alisema kuwa masuala mengi
yanayoleta mgogoro kwenye
Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar yanaibuliwa na wanasiasa.
“Unawezekana kuwa muungano
unatunyima fursa moja ua mbili,
unatunyima uwezo wa kuamua
katika masuala hayo, lakini
wananchi hawayaoni hayo.
Muungano ni wa wananchi, viongozi
wana fursa zao, lakini wahakikishe
wanawahudumia wananchi,”
alisema.
Mjumbe huyo ametoa kauli hiyo siku
chache baada ya Rais Jakaya
Kikwete na baadhi wanasiasa kutoka
CCM, wakiwamo Wajumbe wa Bunge
Maalumu la Katiba kuikosoa Rasimu
ya Katiba Mpya.
Kikwete pamoja na wajumbe hao
kwa nyakati tofauti, walisema kuwa
Rasimu iliyowasilishwa bungeni na
Tume ya Mabadiliko ya Katiba
haionyeshi uhalisia wa matakwa ya
wananchi walio wengi kuhusu
muundo wa muungano.
Akifungua kongamano hilo, Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib
Bilal, alisema kuwa masuala mengi
yanayoleta mgogoro kwenye
Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar yanaibuliwa na wanasiasa.
“Unaweza kuwa muungano
unatunyima fursa moja au mbili,
unatunyima uwezo wa kuamua
katika masuala hayo, lakini
wananchi hawayaoni hayo.
Muungano ni wa wananchi, viongozi
wana fursa zao lakini
wanahakikisha wanawahudumia
wananchi,” alisema.
Akifafanua matumizi ya jina la
Tanganyika kwenye Katiba ya sasa,
Profesa Kabudi alisema: “Katiba ya
Jamhuri ya Muungano ibara ya nne,
34, 64, 102 na 151, inaonyesha kuwa
zipo mamlaka tatu. Mamlaka ya
masuala ya muungano na mamlaka
ya masuala yasiyo ya muungano
katika upande wa Tanzania Bara
(Tanganyika).”
Alibainisha: “Nataka niwaambie, leo
ukienda kwenye Ibara ya 151 ya
Katiba, Tanzania Bara imetajwa
kuwa iliyokuwa Jamhuri ya
Tanganyika, kwa hiyo hata Katiba ya
sasa Tanganyika ipo, kwa hiyo
Tanganyika siyo jina haramu.”
Alisema anaamini kila taifa lina
ujinga wake katika kutunga Katiba,
lakini ujinga wa kizazi kimoja
hauwezi kuwa wa kizazi kingine.
“Ujinga wa kizazi hiki, tusidhani
utakuwa ujinga wa kizazi cha kesho,
vizazi vijavyo vya Tanzania
vitakuwa na ujinga wake.”
Alifafanua: “Ni vyema kuwawekea
misingi lakini waje kuishi na ujinga
wao, kuliko kulazimisha ujinga
wako, kwa sababu wewe ujinga
wako ndiyo amali yako lakini kwa
wengine siyo amali. Ulitegemea
Waingereza wangekapigia mizinga
kachanga ka siku moja?”
Hati ya Muungano
Akizungumzia hati ya muungano
iliyozua sintofahamu hivi karibuni
kwa madai kwamba haikuwepo,
alisema msingi wa kikatiba na
kisheria wa muungano wowote ni
hati za muungano.
Alisema miaka ya 1980, suala
lililokuwa linajadiliwa ni iwapo hati
za muungano ni sehemu ya sheria za
kimataifa au la. Baadaye ilibainika
kuwa hati hizo ni mkataba wa
kimataifa na kwamba unatawaliwa
na sheria za kimataifa.
“Hili suala la kwamba hati zipo au
hazipo siyo suala kubwa, suala
ziliridhiwa? Ushahidi upo upande
wa Tanganyika ziliridhiwa. Kwa
upande wa Zanzibar kuna utata na
hiyo kesi ipo mahakamani,”
alisema.
Alisema kutokana na utata huo
katika Rasimu, wakapendekeza
namna ya kutatua tatizo lililodumu
kwa miaka 50 kwa kuandika kuwa
hati ya maridhiano ya Tanganyika na
Zanzibar kuwa msingi mkuu wa wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Source: TBC via Jamiiforums
Atumia weledi wake katika mambo ya kisheria kuuelezea Muungano.
Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Profesa
Palamagamba Kabudi amejibu
baadhi ya hoja za watu
wanaopendekeza muundo wa
serikali mbili na kusema Serikali ya
Zanzibar ndiyo iliyoanza kutaka
serikali tatu mwaka 1984.”
Aidha, amewashangaa wanaolibeza
jina la Tanganyika kutumika
serikalini kwa madai kuwa jina hilo
siyo haramu kwa kuwa limo ndani
ya Katiba ya sasa.
Alisema kuwa wakati huo madai ya
serikali tatu yalitolewa na Zanzibar
na kusimamiwa na Rais aliyekuwa
pia Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Alhaji Aboud Jumbe.
“Hoja ilipelekwa pia kwenye Baraza
la Wawakilishi, Brigedia Mstaafu
Ramadhan Haji Fakhi (aliyekuwa
Waziri Kiongozi), alikuwa akiongea
kwa sauti nzito, kama ulikuwa
ukimsikiliza, unasema muungano
haupo,” alisema Profesa Kabudi na
kueleza kuwa Fakhi alisema:
“Zanzibar siyo koloni la
Tanganyika.”
Alikuwa akichangia hotuba katika
Kongamano la Kujadili Miaka 50 ya
Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar, lililofanyika mjini
Zanzibar jana. Alieleza kwamba
mjadala wa sasa wa muungano siyo
mkali kama uliokuwepo mwaka 1983
na 1984.
Hata hivyo, hotuba hiyo ya Profesa
Kabudi iliyokuwa ikirushwa moja
kwa moja na Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC1) ilikatishwa kabla
mzungumzaji kumaliza hotuba yake.
Katika maelezo yake, Profesa
Kabudi ambaye pia ni Mhadhiri wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
alisema kuwa Fakhi alikuwa haongei
kama mtu baki, bali aliagizwa na
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
“Lugha ilikuwa ni kali,” alisema.
Akifungua kongamano hilo, Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib
Bilal alisema kuwa masuala mengi
yanayoleta mgogoro kwenye
Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar yanaibuliwa na wanasiasa.
“Unawezekana kuwa muungano
unatunyima fursa moja ua mbili,
unatunyima uwezo wa kuamua
katika masuala hayo, lakini
wananchi hawayaoni hayo.
Muungano ni wa wananchi, viongozi
wana fursa zao, lakini wahakikishe
wanawahudumia wananchi,”
alisema.
Mjumbe huyo ametoa kauli hiyo siku
chache baada ya Rais Jakaya
Kikwete na baadhi wanasiasa kutoka
CCM, wakiwamo Wajumbe wa Bunge
Maalumu la Katiba kuikosoa Rasimu
ya Katiba Mpya.
Kikwete pamoja na wajumbe hao
kwa nyakati tofauti, walisema kuwa
Rasimu iliyowasilishwa bungeni na
Tume ya Mabadiliko ya Katiba
haionyeshi uhalisia wa matakwa ya
wananchi walio wengi kuhusu
muundo wa muungano.
Akifungua kongamano hilo, Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib
Bilal, alisema kuwa masuala mengi
yanayoleta mgogoro kwenye
Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar yanaibuliwa na wanasiasa.
“Unaweza kuwa muungano
unatunyima fursa moja au mbili,
unatunyima uwezo wa kuamua
katika masuala hayo, lakini
wananchi hawayaoni hayo.
Muungano ni wa wananchi, viongozi
wana fursa zao lakini
wanahakikisha wanawahudumia
wananchi,” alisema.
Akifafanua matumizi ya jina la
Tanganyika kwenye Katiba ya sasa,
Profesa Kabudi alisema: “Katiba ya
Jamhuri ya Muungano ibara ya nne,
34, 64, 102 na 151, inaonyesha kuwa
zipo mamlaka tatu. Mamlaka ya
masuala ya muungano na mamlaka
ya masuala yasiyo ya muungano
katika upande wa Tanzania Bara
(Tanganyika).”
Alibainisha: “Nataka niwaambie, leo
ukienda kwenye Ibara ya 151 ya
Katiba, Tanzania Bara imetajwa
kuwa iliyokuwa Jamhuri ya
Tanganyika, kwa hiyo hata Katiba ya
sasa Tanganyika ipo, kwa hiyo
Tanganyika siyo jina haramu.”
Alisema anaamini kila taifa lina
ujinga wake katika kutunga Katiba,
lakini ujinga wa kizazi kimoja
hauwezi kuwa wa kizazi kingine.
“Ujinga wa kizazi hiki, tusidhani
utakuwa ujinga wa kizazi cha kesho,
vizazi vijavyo vya Tanzania
vitakuwa na ujinga wake.”
Alifafanua: “Ni vyema kuwawekea
misingi lakini waje kuishi na ujinga
wao, kuliko kulazimisha ujinga
wako, kwa sababu wewe ujinga
wako ndiyo amali yako lakini kwa
wengine siyo amali. Ulitegemea
Waingereza wangekapigia mizinga
kachanga ka siku moja?”
Hati ya Muungano
Akizungumzia hati ya muungano
iliyozua sintofahamu hivi karibuni
kwa madai kwamba haikuwepo,
alisema msingi wa kikatiba na
kisheria wa muungano wowote ni
hati za muungano.
Alisema miaka ya 1980, suala
lililokuwa linajadiliwa ni iwapo hati
za muungano ni sehemu ya sheria za
kimataifa au la. Baadaye ilibainika
kuwa hati hizo ni mkataba wa
kimataifa na kwamba unatawaliwa
na sheria za kimataifa.
“Hili suala la kwamba hati zipo au
hazipo siyo suala kubwa, suala
ziliridhiwa? Ushahidi upo upande
wa Tanganyika ziliridhiwa. Kwa
upande wa Zanzibar kuna utata na
hiyo kesi ipo mahakamani,”
alisema.
Alisema kutokana na utata huo
katika Rasimu, wakapendekeza
namna ya kutatua tatizo lililodumu
kwa miaka 50 kwa kuandika kuwa
hati ya maridhiano ya Tanganyika na
Zanzibar kuwa msingi mkuu wa wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Source: TBC via Jamiiforums
0 comments :
Post a Comment