Aliyekuwa mlinzi wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ofisa usalama mwandamizi, Aloyce Tendewa, amefukuzwa kazi.
Kwa
mujibu wa gazeti la Mtanzania, Tendewa amefukuzwa kazi na mwajiri wake
ambaye ni Idara ya Usalama wa Taifa (TIS) kwa kosa la kushindwa
kutekeleza majukumu yake ya kikazi.
Mbali
na taarifa hizo, imeelezwa pia kuwa sababu nyingine ya kufukuzwa kwake
kazi kwa mwanausalama huyo ambayo hata hivyo haijathibitishwa, ni madai
ya kutoa taarifa za kubadilishiwa kituo chake cha kazi cha awali.
Inadaiwa
kuwa Tendewa baada ya kuvuliwa jukumu la kumlinda Lowassa alibaki na
kinyongo moyoni kwa sababu hakuridhika na hatua hiyo hivyo alivujisha
taarifa hizo kwa vyombo vya habari jambo lililoelezwa kuwa ni kinyume na
maadili ya kazi yake.
Inadaiwa kuwa Tendewa alipewa barua ya kuachishwa kazi juzi jioni baada ya kuvuja kwa uhamisho wake kwenye vyombo vya habari.
“Alikuwa
bado anataka kuendelea kumlinda mzee (Lowassa), lakini kuna vitu
alishindwa kuvitekeleza kwa ufasaha kwa hiyo kitendo cha kuondolewa
kilimuudhi akaamua kupeleka taarifa gazetini jambo ambalo ni kinyume na
taratibu zao za kazi za kiusalama,” alidokeza mmoja wa maofisa
Kwa
upande mwingine taarifa zinaeleza kuwa mpango wa kutimuliwa kwa Tendewa
uliandaliwa kwa muda wa miezi kadhaa na barua ya kufukuzwa iliandikwa
baada tu ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.
Kwamba,
pamoja na sababu nyingine Tendewa anadaiwa kushindwa kuwasiliana
inavyotakikana na viongozi wake kuhusu majukumu yake ya kiulinzi wakati
akiwa mlinzi wa Lowassa.
Taarifa
zinadai, kushindwa huko kwa Tendewa kuliwafanya viongozi wake kufikia
uamuzi wa kumfukuza kazi na kwamba barua yake iliandikwa mapema Desemba
mwaka jana, lakini hakukabidhiwa hadi hivi karibuni alipovujisha siri za
kuhamishwa kwake kituo cha kazi.
Mmoja
wa watoa habari aliyeko serikalini ameeleza kuwa Tendewa aliundiwa
kamati ya kumchunguza kuhusu kushindwa kutekeleza majukumu sawasawa
ambayo ilifanya kazi kwa muda wa wiki mbili na kuwasilisha ripoti yake
makao makuu.
Hata
hivyo, alisema bado kuna utata kuhusu mtu aliyesaini barua ya kufukuzwa
kazi kwa Tendewa ambaye kwa wadhifa wake ilipaswa kusainiwa na
Mkurugenzi Mkuu lakini badala yake imesainiwa na ofisa wa cheo cha
chini.
Tendewa amefukuzwa kazi akiwa amebakiza mwaka mmoja kustaafu utumishi wake katika Idara ya Usalama wa Taifa.
Rekodi
za utendaji kazi wa Tendewa zinaonyesha kuwa baada tu ya kuajiriwa na
TIS, alipelekwa katika kikosi cha walinzi wa hayati Mwalimu Julius
Nyerere na kutokana na uhodari wake aliaminiwa na Mwalimu.
Aidha,
rekodi hizo zinaonyesha kuwa Tendewa ni miongoni mwa wana usalama
wachache waliopigana vita ya kumng’oa aliyekuwa Rais wa Uganda, Fashisti
Iddi Amini Dada mwaka 1978 na 1979 na akiwa vitani alitekwa na kwenda
kuzuiliwa nchini Sudan.
Historia
hiyo inaonyesha kuwa Tendewa aliokoka kuuawa kwa risasi akiwa mateka
muda mfupi baada ya kurejeshwa nchini kutoka Sudan siku chache baada ya
Rais Yoweri Museveni kushika madaraka ambapo mmoja wa walinzi wanawake
wa rais alimuona na kumtambua kuwa alikuwa mmoja wa wapiganaji hodari wa
Tanzania na si muasi kama ilivyokuwa ikidhaniwa hivyo alirudishwa
Tanzania.
Baada
ya kurejeshwa nyumbani alipewa jukumu la kuwa mlinzi wa Mwalimu Nyerere
na hata alipong’atuka madarakani aliendelea na kazi hiyo hadi Mwalimu
alipofariki dunia katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas London nchini
Uingereza.
Chanzo: Mtanzania
Mpekuzi blog
0 comments :
Post a Comment