Wakati AS Saint-Étienne wakiwa wameweka offer mezani kwa TP Mazembe ya kumtaka Thomas Ulimwengu, mashabiki wa Besiktas FC wameingiwa na wazimu wakimtaka Ulimwengu kwa udi na uvumba ili nyota huyo ajiunge na timu yao inayoongoza ligi kuu ya Uturuki ‘Super Lig’.
Tayari klabu ya Étienne ya Ufaransa imeshapeleka offer rasmi kwa klabu ya TP Mazembe ikimtaka nyota huyo wa Tanzania ajiunge nayo na tayari Mazembe wako tayari kumwachia Ulimwengu endapo watafikia makubaliano ya pande zote mbili.
Mashabiki wa Besiktas wamepost picha za Ulimwengu kwenye mitandao ya kijamii wakimkaribisha na kumshawishi ‘Uncle Thom’ ajiunge na klabu yao.
Tukio hilo si la ajabu kutokea kwani Samatta kwenye moja ya interviews zake na mtandao huu alisema kwamba, yeye alisajiliwa TP Mazembe kwa nguvu ya mashabiki ambao walishuhudia kiwango chake kwenye mchezo kati ya Simba SC dhidi ya TP Mazembe mchezo wa klabu bingwa uliochezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Samatta anasema mashabiki wa Mazembe waliushinikiza uongozi chini ya Moise Katumbi kumsajili yeye na billionaire huyo wa Congo DR akamsajili Samatta kama mashabiki wa timu yake walivyopendekeza.
Endapo uongozi wa Besiktas FC utaamua kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuiwania saini ya Ulimwengu, itaingia moja kwa moja kwenye mchuano na klabu ya AS Saint-Étienne kumuwania mchezaji huyo na hapo Mazembe wataangalia ni klabu gani kati ya hizo mbili ambayo itatoa dau la maana kwa ajili ya kumnasa Ulimwengu.
0 comments :
Post a Comment