SAMATTA: Tuzo Yangu Nai-Dedicate Kwa Mh JAKAYA KIKWETE
Mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika Anayecheza ndani ya mipaka ya bara hili - Mbwana Samatta amesema tuzo yake hii anai-dedicate kwa Raisi Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania @JK kwete pamoja na Watanzania kiujumla.
Mbwana alisema: "Nakosa la kusema kwakweli, kwa jinsi watanzania walivyokuwa wameniombea na kwa tuzo hii sijui hata nisemaje ili kuwashukuru au sijui nifanyaje kuwashukuru ili wajue kweli nawapenda na niko nao pamoja kwasababu ya maombi na jinsi walivyokuwa wanaonesha imani hata ambayo mimi mwenyewe sikuwa nayo kwenye hii tuzo.
Lakini pia sidhani kama naweza kumsahau Rais mstaafu Mh. Jakaya Mrisho Kikwete kwa inspiration ambayo alinipa siku moja ambayo tulikutana nchini Congo DR aliniambia mambo mengi sana ambayo kwa kiasi kikubwa yalini-motivate.
Unajua mtu kama Rais anakuja anakwambia mambo ambayo yanakuhusu moja kwa moja na taifa ni jambo kubwa.
Mbwana Samatta: Ni mengi tulizungumza lakini moja alituambia mimi na Thomas kwamba, tumeonesha njia tusikubali kubakia Afrika tujitahidi kwenda kucheza Ulaya ili kuonesha njia kwa vipaji vingine ambavyo viko nyumbani.
Alisema nyinyi ndio icons wetu, watanzania karibu wote tunawategemea nyinyi kwenye medani ya soka, mjitahidi msituangushe.
Sidhani kama hata wewe mwenyewe nikikwambia unachukuliaje lakini ni maneno ambayo kwa kiasi kikubwa yalini-push kwa kuona ikiwa Rais anasema hivi, je familia yangu au watu wa karibu pamoja na sehemu niliyotokea wanachukuliaje hili suala lakini ilinipa morali na kusema kweli inabidi nifanye vizuri. Kweli nashukuru Mungu amenisaidia.

0 comments :
Post a Comment