-->

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA IJUMAA 08.01.2016


Real Madrid wanatazama uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane, 22, katika mradi wao wa kujenga upya timu (Daily Telegraph), Manchester United watajaribu kumsajili Eden Hazard, 25 kutoka Chelsea kwa pauni milioni 65, baada ya kuambiwa na Real Madrid kuwa Gareth Bale, 26, hauzwi (Daily Star), meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane atataka kumsajili Eden Hazard, lakini Hazard mwenyewe atasubiri kwanza kuona nani atakuwa meneja wa kudumu wa Chelsea (Daily Telegraph), kuwasili wa Didier Drogba kama kocha Chelsea huenda kukamfanya Hazard asiondoke Stamford Bridge (Daily Express), Chelsea walimtaka Carlo Ancelotti, 56, kuchukua nafasi ya Jose Mourinho, 52, wiki tano kabla hawajamfukuza Mourinho, lakini Ancelotti hakutaka mkataba wa muda mfupi (Daily Mail), Manchester United wametupilia mbali taarifa kuwa wanataka kumsajili mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku, 22, mwezi huu, lakini wako tayari kutoa pauni milioni 40 kumnunua mwisho wa msimu (Daily Mirror), Man United wameambiwa na Lazio watoe pauni milioni 36 kumnunua winga kutoka Brazil Filipe Anderson, 22 (Sun), meneja wa Everton Roberto Martinez amesema hakuna makubaliano yoyote na beki wa kati, John Stones, 21, na kuwa anaweza kuondoka mwisho wa msimu (Daily Star), Chelsea ni miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyomnyatia kiungo mwenye umri wa miaka 12 wa Barcelona, Xavi Simons, na tayari wamewasiliana na baba wa mtoto huyo (Daily Mail), matumaini ya Liverpool na Manchester United ya kumsajili Ilkay Gundogan, 25, kutoka Borussia Dortmund yamefufuka, baada ya Juventus kuacha kumfuatilia mchezaji huyo (Daily Express), Stoke City huenda wakapanda dau kumtaka Saido Berahino, 22, kutoka West Brom (Guardian), beki Jan Kirchkoff, 25, amesema alikataa kwenda katika timu tatu za Bundesliga, kabla ya kuamua kuhamia Sunderland akitokea Bayern Munich (Sunderland Echo), Napoli wamekataa dau la pauni milioni 14 kutoka Swansea la kumsajili Manolo Gabbiadini, 24 (Guardian), meneja wa Crystal Palace Alan Pardew amesema hana mpango wa kumsajili Emmanuel Adebayor, 31, ambaye ni mchezaji huru (Croydon Advertiser). Habari zilizothibitishwa, nitakujuza. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema!!
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment