*Real wamtaka Hazard
*Aubameyang kwenda Arsenal?
*Juventus wamsaka Herrera
Real Madrid wapo tayari kutoa pauni milioni 100 kumsajili Eden Hazard, 24 kutoka Chelsea (Daily Star), hatua hiyo huenda ikaifanya Chelsea ianze kumtaka Gareth Bale, 26, wa Real Madrid (Daily Mirror), Lakini Manchester United wana matumaini ya kumsajili Bale kwa pauni milioni 75 mwezi huu ili aweze kufanya kazi na Giggs ambaye pia anatoka Wales kama Bale (Daily Mail), Bale hana mipango ya kuondoka Real Madrid baada ya kufukuzwa kwa Benitez, lakini hatma yake itategemea zaidi nafasi atakayochezeshwa na Zinedine Zidane (Guardian), meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola, 44, atakuwa meneja mpya wa Manchester City msimu ujao (Sky Sports), iwapo Guardiola atakwenda City, klabu hiyo itataka kumsajili Lionel Messi, 28 wa Barca (Daily Express), Guardiola pia huenda akajiunga na Manchester United iwapo watachangamka. Kocha huyo amezungumza na vilabu vyote viwili vya Manchester, amekataa dau la Chelsea, lakini pia atakuwa tayari kuifikiria Arsenal (Sun), mwandishi mkuu wa michezo wa Daily Mail, John Cross anaamini mkataba kati ya Guardiola na Manchester City "umekamilika" (BBC Radio 5 live), meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini anasema atakubali kufukuzwa kazi hata kama akishinda Ligi Kuu (Daily Mirror), mshambuliaji wa zamani wa Tottenham, Emmanuel Adebayor, 31, amepata dau kutoka Watford na Crystal Palace (Guardian), Chelsea wanasitasita kumwachilia Loic Remy, 29, anayesakwa na Newcastle, Aston Villa na Crystal Palace (Daily Mail), Watford wanakaribia kumsajili kiungo kutoka Spain, Mario Suarez, 28, anayeichezea Fiorentina (Daily Star), uhamisho wa kiungo wa FC Basel Mohamed Elneny kwenda Arsenal utakamilika hivi karibuni (London Evening Standard), kiungo wa AC Milan, Nigel de Jong, 31, hatafutwi na Leicester, licha ya taarifa kuzagaa (Leicester Mercury), winga kutoka Ebelgiji, Kevin Mirallas, 28, hatoondoka Everton kwa mujibu wa Roberto Martinez (Talksport), Everton wanatazamia kumsajili Shani Tarashaj, 20 kutoka Grasshopper ya Uswisi (Liverpool Echo), mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre- Emerick Aubameyang alikosa mazoezi siku ya Jumanne. Mchezaji huyo amehusishwa na kuhamia Arsenal na Liverpool (Independent), Tottenham watampa Delle Alli mkataba mpya na kuongeza mshahara wake kufikia pauni 20,000 kwa wiki (Evening Standard), Juventus wanajiandaa kupanda dau kumtaka kiungo wa Manchester United Ander Herrera (Fishajes.net). Uhamisho uliothibitishwa, nitakujuza. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Tafadhali share hizi na wapenda soka wote. Siku njema!!
0 comments :
Post a Comment