Thomas Ulimwengu ‘Drogba wa Dodoma’ amejikuta akishindwa kutoa neno kwa pacha wake Mbwana Samatta, kutokana na furaha aliyokuwa nayo baada ya Samatta kunyakua tuzo ya mchezaji bora Afrika 2015 kwenye tuzo za Glo-Caf Awards zilizofanyika usiku wa January 7, 2016 Abuja, Nigeria.
Samatta na Ulimengu wamecheza kwa pamoja na kwa mafanikio makubwa sana kwenye klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Ulimwengu ame-post kwenye account yake ya twitter ujumbe unaoashiria furaha yake kufuatia Samatta kutwaa tuzo hiyo.
Wawili hao walikuwa miongoni mwa kikosi kilichocheza michezo yote miwili ya fainali ya klabu bingwa Afrika na kufanikiwa kutwaa ndoo hiyo ambapo waliweka rekodi ya kuwa watanzania wa kwanza kunyakua kombe hilo kubwa na lenye heshima kubwa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.
Ujumbe wa Thomas Ulimwengu ulisomeka: “Nashindwa kuonyesha hisia zangu, kwa tuzo kubwa kama hii uloipata pacha..Hongera sana @samagoals Mungu ametimiza maombi yetu..”, hayo ni maneno yaliyoandikwa kwenye account ya twitter ya Thomas Ulimwengu.
Kwenye post hiyo Ulimwengu ame-post pia picha ya zamani akiwa pamoja na Mbwana Samatta na kuandika maneno haya, “..#throwBack#hainakufeli#2016#LetThisBeOurYear”.
Samatta ameingia kwenye rekodi za vitabu vya Afrika kutokana na kutwaa tuzo hiyo pamoja na kuiwakilisha vyema Tanzania.
0 comments :
Post a Comment