-->

KISA CHENYE MAFUNZO

Mwalimu mmoja aliita wanafunzi wake akawaambia''Kesho kila mwanafunzi aje na nyanya kulingana na idadi ya watu anaowachukia, Yani kama unamchukia mtu mmoja uje na nyanya moja kama ni wawili basi njoo na nyanya mbili hivyo hivyo.
Nyanya hizo mtazibeba kwenye mabegi yenu ya kubebea madaftari na vitu vingine vya shule
''Wanafunzi wakakubali afu kesho yake wanafunzi wakazibeba zile nyanya vizuri kabisa wengine walibeba moja,wengine mbili na wengine nyingi sana.
Kama mwalimu alivyosema zile nyanya zikapewa majina ya watu ambao wanafunzi wanawachukia.
Baada ya kuzipa hizo nyanya majina mwalimu akawaambia kila mwanafunzi azirudishie nyanya zake kwenye begi lake afu aziache humo humo ndani ya begi kila siku awe anakuja nazo shuleni na kurudi nazo.
Baada ya siku kadhaa wanafunzi wakaanza kulalamika hasa wale waliobeba nyanya nyingi kuwa nyanya ni nzito sana na zinatoa harufu mbaya na zinaharibu vitu vyao vizuri walivyoweka kwenye mabegi. Mwalimu akawaambia hivi ndivyo ilivyo mtu unapoweka watu moyoni usiowapenda. kama mtu huwezi kuvumilia kukaa na harufu ya nyanya kwenye begi vipi kuhusu madhara ambayo moyo unayapata kwa kuubebesha mzigo wa chuki dhidi ya watu.? Moyo unapata madhara makubwa sana unapobebeshwa chuki kila wakati kila siku moyo unakuwa na chuki na hapo ndipo unaharibika na kusababisha kuharibu hata vitu vingine vizuri vilivyokuwa moyoni. Moyo ni kama lile begi la kubebea madaftari unahitaji kubeba vitu vizuri na Visalia.
Safisha moyo kwa kusamehe wanaokukosea, jifunze kusamehe mana ni moja ya virutubisho vya moyo wako.

Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment