Mbwana Samatta ndio jina liliotajwa zaidi
kwenye vinywa vya watanzania wengi na Afrika
kiujumla ndani ya masaa kadhaa yaliyopita –
baada ya mwanasoka huyo wa Kitanzania
anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe
kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika
Anayecheza Ligi za Ndani ya Afrika.
Ushindi wa Samatta, ambaye ni mshindi wa na
mfungaji bora wa ligi ya mabingwa wa Afrika
umetokana na kuwashinda wapinzani wake Zein
Edin Farahat, Roger Assale, Robert Kidiaba,
Moudather el Tahir,Mohammed Meftah, Kermit
Erasmus, Felipe Ovono, Baghdad Bournedjah, na
Abdeladim Khadrouf.
Utaratibu wa CAF – Shirikisho la soka katika
upigaji kura wa kumchagua mshindi wa tuzo hii
unatokana na kura zilizopigwa na makocha wa
timu za taifa au wakurugenzi wa ufundi wa
vyama vya soka vya nchi za kiafrika.
Kwa mwaka huu wachezaji wote hao waliotajwa
hapo juu walipigiwa kura na matokeo ni kama
yanavyoonekana kwenye mpangilio hapo chini.
Mbwana Samatta alipata jumla ya kura 127 na
hivyo kuongoza, akifuatiwa kwa mbali na
mchezaji mwenzie wa TP Mazembe Robert
Kidiaba aliyepata kura 88 na aliyefunga Top 3 ni
Baghdad Bournedjah. Kura zilipigwa na mataifa
45 ya nchi wanachama wa shirikisho la soka
Afrika CAF.
HONGERA SANA MBWANA SAMATTA KWA KUWATOA KIMASOMASO WATANZANIA
Home
/
featured
/
michezo
/
MBWANA SAMATTA ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRICA KWA WANAOCHEZA NDANI YA AFRICA
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment