-->

WALIMU NA HARAKATI ZA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA.



Harakati za uhuru zimefanyika karibu nchi zote za Afrika,Tanganyika ni moja miongoni mwa nchi zilizotawaliwa na wakoloni wa Kijerumani na baadae wa kiingereza baada ya vita ya kwanza ya dunia.
Kwa miongo kadhaa nchi za Afrika zimekuwa chini ya uatawala wa kikoloni.Kipindi hiki cha Ukoloni kilikuwa kipindi kigumu sana kwa Waafrika kilichohusisha adha za kila aina.
Kwa Waafrika hawakupendezwa na ujio wa wakoloni,Hivyo toka awali Wafrika walianza kuonyesha hasira zao dhidi ya wavamizi katika ardhi yao tukufu.
Baada ya kipindi kirefu cha mateso na taabu kwenye kipindi cha ukoloni ndipo walipoibuka wanaharakati mbali mbali wa kupigani uhuru.
Harakati za kupigania uhuru zilianza tangu pale tu wakoloni walipoingia ingawaje harakati hizo za awali hazikuratibiwa kwa uzuri,pia hazikuongozwa na wasomi na nyingi ya harakati hizo zilifanywa kikabila Zaidi kuliko kitaifa.
Baada ya vita ya kwanza ya dunia harakati madhubuti za kupigania uhuru zilianza na baada ya vita ya pili ya dunia harakati hizi zilipamba moto safari hii zikiongozwa na wasomi pamoja na wazalendo waliotoka kupigana vita vya kwanza na vita vya pili vya dunia.
Wasomi wa kada mbali mbali walishiriki harakati za ukombozi wa Tangayika lakini Makala hii imejikita kwenye mchango wa walimu katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Walimu ni watu ambao wanakutana na watu wengi kwa wakati mmoja na hupata muda mwingi wa kuzungumza nao hivyo huweza tumia nafasi hiyo kupandikiza kile ambacho mwalimu anakiamini.
Mbali na vipawa vya kuzaliwa navyo lakini walimu wamejifunza saikolojia za watu hivyo hutumia nyenzo hiyo kama sehemu ya ushawishi na kukamilisha lile ambalo mwalimu anataka liwafikie watu,mfano kwenye filamu ya Sarafina Mwalimu Mary Masombuko alikuwa mwalimu mwenye ushawishi mkubwa na kufanikmiwa kupandikiza hisia za kizalendo kwa watoto wa kiafrika.
Katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika safari inaanza na Mwalimu Cecil Matola ambaye alikuwa mmoja ya waanzilishi wa African Association katika miaka ya 1927 pia vitabu vingine vimeandika 1929.Mwalimu Cecil Matola alipata braka zote za aliyekuwa gavana wa Uingereza kwa kipindi kile Sir David Cameroon.TAA iliundwa na watu 9 akiwemo Mwalimu Cecil Matola,Kleist Sykes,Mzee Bin Sud,Ibrahim Hamisi,Zibe Kidasi,Ali Said Mpima,Suleiman Majisu,Raikes Kusi na Rawson Watts.Mwalimu Cecil Matola mabaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa African Association alifariki dunia mwaka 1933 na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa katibu wake Ndugu Kleist Sykes.
Mwlimu James Aggrey ,Huyu ni mgana ambaye alikuatana na Kleist Sykes wakati huo Kleist Sykes ametoka vitani na akawa anafanya kazi Tanganyika Railways.Dr James Aggrey inasemekana ndiye aliyemuamasisha Kleist Sykes kwenda kuanzisha African Association ambayo baadae ikawa TAA kisha TANU.
Mwalimu Thomas Sauti Plantan,Huyu atakumbukwa kwa nafasi yake ya uraisi wa TAA miaka 1950s,katibu wake akiwa Mzee Clement Mohammed Mtamila walikumbana na mtihani wa kupinduliwa kwenye uongozi na vijana.Baada ya kupinduliwa kwenye madaraka Dr Vedasto Kyaruzi akawa rais wa TAA na Abdulwahiid Sykes mtoto wa Kleist Sykes akawa ndio katibu wake.
Mwalimu Kahere wa Tanga,Huyu atakumbukwa katika mchakato wa safari ya mwalimu Nyerere ya mwaka 1955 kwenda UNO Kwa ajili ya kudai Uhuru.Itakumbuka kuwa nauli ya kwenda Marekani wakati ule ilikuwa shilingi 12,000.Watu mbali mbali walichangia nauli pamoja na maradhi ya Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kwenda UNO. Lakini pesa hazikutosha na ndipo Mwalimu Kahere wa Tanga alipowaambia viongozi wa TANU waende Tanga kuchukua pesa.Special branch(usalama wa taifa wa zama za mkoloni) walitaka kuzuia upatikani wa pesa hizo lakini walishindwa na hatimaye Idd Faizi Mafongo alifanikiwa kuzikabdidhi pesa kwa viongozi wa TANU na hatimaye Mwalimu Nyerere akaenda UNO tarehe 05/03/1955 ingawaje habari hii inapingana na anachoeleza Yericko Nyerere kwenye kitabu chake cha Ujasusi wa Kidola(2016) kwamba kwamba kanisa katoliki lililipia nauli ya tiketi ya ndege kwa kwenda na kurudi.
Mwalimu Kambarage Julius Nyerere,huyu ndio shujaa wa mwisho kwa walimu ambaye alifunga safari ya kwenda Umoja wa mataifa kwenda kudai uhuru wa Tanganyika na kwa jitihada zake huku akishirikiana na viongozi wengine wa TANU uhuru wa Tanganyika ulipatikana tarehe 9/12/1961.
Mwalimu Nyerere amefanya mambo mengi kutoka uhuru mpaka kifo chake kilichotokea tarehe 14/10/1999 katika hospitali St. Thomas huko nchini Uingereza.
Hivyo leo katika kumbukumbu ya kifo cha mwalimu Nyerere na pia tunawakumbuka wazalendo wengine ambao kwa namana moja au nyingine walifanikisha upatikanaji wa uhuru wa Tanganyika ingawaje wamesahaulika kwenye vitabu vyetu(kiada na ziada) vya kuwafundishia watoto mashuleni.
Makala hii imeandikwa kwa rejea za kitabu kiitwacho Maisha ya Abdulwahiid Sykes,Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi,ripoti ya Tadasu TSURUTA na mtandao wa wikipedia
Ndimi
MWALIMU OMARI A MAKOO
Whatsapp no:+255714557223
Umar.makoo@gmail.com
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment