Polisi wanasema kuwa Monsignor Nunzio Scarano, anakabiliwa na kosa lengine la kupanga njama ya kuingiza kiharamu dola milioni 26 nchini Italia na kwamba yuko chini ya kifungo cha nyumbani.
Mhasibu huyo wa zamani wa Vatican na watu wengine wawili, walipokea kibali cha kukamatwa siku ya Jumanne.
Mwaka jana Papa Papa Francis aliunda tume, ya kutathmini shughuli za kanisa hilo baada ya kashfa kadhaa kujitokeza kuhusu kanisa hilo.
Vatican imekataa ombi la idara ya mahakama ya Italia kuchunguza madai hayo, yaliyotendwa na maafisa hao kwa misingi ya kidiplomasia.
Lakini chini ya uongozi wa Papa Francis, ushirikiano umeimarika kati ya Maafisa wa Italia na Vatizan ambao ulipelekea kukamatwa kwa Kasisi Monsignor Scarano, majira ya joto.
Mnamo Jumanne polisi walipata Euro milioni 6.5 katika akaunti ya benki pamoja na katika nyumba ya Kasisi Monsignor Scarano mjini Salerno.
Maafisa wakuu wanasema kwamba mashitaka ya sasa hivi dhidi ya Monsignor Scarano ni kuhusu kutoa michango bandia ambayo inasemekana ilitoka katika benki zingine kimataifa.
CHANZO:MSHANA JUNIOR
0 comments :
Post a Comment