-->

AL SHABAAB WAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA INTERNET MOBILE NA FIBER OPTIC

somalimemo.netHarakat Al Shabab Al Mujahideen imetoa Tamko inayowahusu mashirika ya Mawasiliano nchini Somalia,ambapo inapiga marufuku baadhi ya huduma zinazotolewa na Mashirika hayo.


Katika Tamko hilo ilisema kuwa Harakat Al-Shabab Al Mujahideen kwanzia sasa imepiga Marufuku utumiaji wa Huduma ya Internet kwenye simu za Kiganjani yani (Mobile Internet) pamoja na Huduma ya Internet Fiber Obtic iliyo na Kasi ya hali ya juu ya Interenet.



Baadhi ya Vipengele viliyomo kwenye Tamko kwa Mashirika ya Mawasiliano nchini Somlai ni kama yafuatayo.



1. Kusimamishwa Mara mmoja huduma ya Internet kwa Utumiaji wa Simu za Kiganjani yani Internet Mobile na Huduma ya Fiber Optic Nchini Somalia.


2. Mashirika yote inayohusu utoaji wa Huduma hizo za Internet Mobile na Fiber Optic kusimamisha mara mmoja.


3. Mashirika yote inayohusiana na utoaji wa Huduma tulizozitaja hapo juu zina siku 15 tu ya kuusimamisha Huduma hizo za Internet Mobile na Fiber Optic,Muda huo ambayo inaanzia tangu Tamko hili ilipotolewa.


4. Mahirika au mtu yeyote atakaye shindwa kutekeleza Amri hii ataonekana anafanya kazi pamoja na Maadui,na atachukuliwa hatua za Kisheria inayomstahiki kwa kuzingatia sheria za Kislaam.
CREDIT TO:SOMALIMEMO
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment