-->

HII NDIO POST YA MH ZITTO KABWE BAADA YA TAIFA KUONDOKEWA NA MTU MASHUHURI NA MCHAPAKAZI DK WILLIAM MGIMWA

Tanzia Waziri wa Fedha William Mgimwa, Mb

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Waziri wetu wa Fedha ndg. William Mgimwa.
Kwa kipindi kifupi nilichofanya naye kazi kwa karibu, kwanza kwenye Kamati ya Fedha (nikiwa mkaribishwa kama Waziri wa Fedha kivuli), kisha kwenye kamati ndogo niliyounda kuhusu miradi ya Umeme ya Mchuchuma na Liganga na Ngaka, na baadaye akiwa Waziri wa Fedha, jambo la msingi nilioona kwake ni unyenyekevu na heshima kubwa aliyonayo kwa watu wengine. Hakusita kuomba ushauri licha ya kuwa na tofauti za kivyama na kwa kweli ni Waziri wa Fedha niliyeelewana naye zaidi kuliko wengine wote waliopita nikiwa ama Waziri Kivuli au Mwenyekiti wa Kamati za Mahesabu. Uzalendo wake hauna mashaka na kujituma kwake katika kazi ni tabia ya kupigiwa mfano.
Mungu ameamua kumchukua mja wake na sisi wanadamu hatuna uwezo wa kupinga. Nawapa pole sana familia yake kwa kumpoteza baba yao mpendwa. Naomba mola awape moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.
Nawapa pole wananchi wa Jimbo la Kalenga na Halmashauri ya Wilaya Iringa kwa kupoteza kiongozi wao.
Mola ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment