-->

ARSENAL WAFANYA KWELI NA KUENDELEA KUSHIKILIA MSKANI WA LIGI KUU UINGEREZA

Mchezaji wa  Arsenal Santi Cazorla akishangilia bao lake huku akikimbizwa kupongezwa na  Olivier Giroud baada ya kuiwasha  Fulham leo jumamosi jioni kwenye mchezo wa Ligi kuu England. Kipindi cha Kwanza Timu zote mbili hazikuweza kufungana hivyo kulazimika kwenda mapumziko zikiwa 0-0, Kipindi cha pili dakika ya 57 ndipo Arsenal walipoanza kufungua lango la Fulham, Bao la kwanza likifungwa na Santi Cazorla baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Jack Wilshere na bao la pili likifungwa tena na huyo huyo Santi Cazorla katika dakika 62 kwa kupata krosi tena kutoka kwa Monreal na hatimaye akaachia shuti akiwa ndani ya box na kummaliza kipa wa Fulham. 
Mesut Ozil chupuchupu amfunge kipa wa Fulham Maarten Stekelenburg

Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment