Mwanasheria makini Ndg. Albert
Msando amewatoa nishai mawakili
watatu wa chadema: Peter Kibatala,
Tundu Lissu na John Mallya. Watoka
mahakamani kwa aibu, Kamati kuu
yapigwa marufuku kumjadili Zitto
Kabwe, waogopa kumjadili Samson
Mwigamba na Dr. Kitila Mkumbo.
Kivumbi na jasho mahakamani leo –
Lissu aumbuka Zitto Kabwe alitinga tena
leo mahakamani na wakili wake Albert
Msando wakati kesi yake dhidi ya bodi
ya wadhamini Chadema na Katibu Mkuu
wa Chadema ilipoendelea Mahakama
Kuu ya Tanzania. Leo maombi
yamesikilizwa na pande zote mbili
zilipata nafasi ya kutoa maelezo yao. Jaji
alianza kwa kutoa maelezo ya sababu
zake za kutupilia mbali jana pingamizi za
mawakili wa Chadema na kutoa amri ya
kuzuia kamati kuu ya Chadema kujadili
suala la Zitto Kabwehadi shauri hili la leo
likamilike.
Katika majibizano marefu, mawakili 3 wa
Chadema walitoa hoja zao na
Mwanasheria wa chama Tundu Lissu
alidai kuwa lengo la Kamati Kuu ni
kuchunguza kama Zitto ana sifa ya kuwa
mwanachama wa Chadema na kuna
uwezekano wa kumsimamisha kwa
muda, kumpa adhabu au hata
kumsamehe Zitto na si kumfukuza tu.
Hata hivyo wakili msomi Albert Msando
alimumbua kwa kielelezo cha barua ya
chama kwa Zitto ya tarehe 26 Novemba
iliyomwita kujieleza katika kikao cha
Kamati Kuu ambayo ilimtaka ajitetee
dhidi ya azimio la Kamati Kuu la
kumwachisha au kumfukuza
uanachama.
Wakili Msando alieleza kuwa barua hiyo
imeonyesha wazi nia ovu ya Kamati Kuu,
ilhali bado rufaa aliyokata mteja wake
Zitto Kabwe haijasikilizwa. Lissu pia
alijaribu kupotosha mahakama kwa
kutumia hoja ambayo pia walisambaza
kama ujumbe wa simu za mkononi kuwa
kesi hii ingesimamisha shughuli zote za
chama. Wakili Msando alifafanua kuwa
kesi hii ni ya kutaka kupata zuio ili suala
la uanachama wa Zitto lisijadiliwe mpaka
atakapopata haki yake ya rufaa ndani ya
chama kama alivyoomba katika barua
yake ya tarehe 10 Desemba. Na zuio hilo
si la kuzuia shuguli za chama.
Wakili Msando alisisitiza pia kuwa
mpaka leo hii hata mwenendo wa kikao
cha kamati kuu hajapatiwa Zitto wala
kujibiwa kinyume na katiba ya chama.
Tundu Lissu alitoa hoja dhaifu kuwa
kuchelewa kwa utaratibu kama huu ni
kawaida katika taasisi. Lakini wakili
Msando alisema kutojibu kabisa barua
yao ni ishara nyingine ya nia ovu ya
Kamati Kuu. Jaji John Utamwa
aliahirisha kutoa uamuzi mpaka
Jumatatu 06/01/2014
Msando amewatoa nishai mawakili
watatu wa chadema: Peter Kibatala,
Tundu Lissu na John Mallya. Watoka
mahakamani kwa aibu, Kamati kuu
yapigwa marufuku kumjadili Zitto
Kabwe, waogopa kumjadili Samson
Mwigamba na Dr. Kitila Mkumbo.
Kivumbi na jasho mahakamani leo –
Lissu aumbuka Zitto Kabwe alitinga tena
leo mahakamani na wakili wake Albert
Msando wakati kesi yake dhidi ya bodi
ya wadhamini Chadema na Katibu Mkuu
wa Chadema ilipoendelea Mahakama
Kuu ya Tanzania. Leo maombi
yamesikilizwa na pande zote mbili
zilipata nafasi ya kutoa maelezo yao. Jaji
alianza kwa kutoa maelezo ya sababu
zake za kutupilia mbali jana pingamizi za
mawakili wa Chadema na kutoa amri ya
kuzuia kamati kuu ya Chadema kujadili
suala la Zitto Kabwehadi shauri hili la leo
likamilike.
Katika majibizano marefu, mawakili 3 wa
Chadema walitoa hoja zao na
Mwanasheria wa chama Tundu Lissu
alidai kuwa lengo la Kamati Kuu ni
kuchunguza kama Zitto ana sifa ya kuwa
mwanachama wa Chadema na kuna
uwezekano wa kumsimamisha kwa
muda, kumpa adhabu au hata
kumsamehe Zitto na si kumfukuza tu.
Hata hivyo wakili msomi Albert Msando
alimumbua kwa kielelezo cha barua ya
chama kwa Zitto ya tarehe 26 Novemba
iliyomwita kujieleza katika kikao cha
Kamati Kuu ambayo ilimtaka ajitetee
dhidi ya azimio la Kamati Kuu la
kumwachisha au kumfukuza
uanachama.
Wakili Msando alieleza kuwa barua hiyo
imeonyesha wazi nia ovu ya Kamati Kuu,
ilhali bado rufaa aliyokata mteja wake
Zitto Kabwe haijasikilizwa. Lissu pia
alijaribu kupotosha mahakama kwa
kutumia hoja ambayo pia walisambaza
kama ujumbe wa simu za mkononi kuwa
kesi hii ingesimamisha shughuli zote za
chama. Wakili Msando alifafanua kuwa
kesi hii ni ya kutaka kupata zuio ili suala
la uanachama wa Zitto lisijadiliwe mpaka
atakapopata haki yake ya rufaa ndani ya
chama kama alivyoomba katika barua
yake ya tarehe 10 Desemba. Na zuio hilo
si la kuzuia shuguli za chama.
Wakili Msando alisisitiza pia kuwa
mpaka leo hii hata mwenendo wa kikao
cha kamati kuu hajapatiwa Zitto wala
kujibiwa kinyume na katiba ya chama.
Tundu Lissu alitoa hoja dhaifu kuwa
kuchelewa kwa utaratibu kama huu ni
kawaida katika taasisi. Lakini wakili
Msando alisema kutojibu kabisa barua
yao ni ishara nyingine ya nia ovu ya
Kamati Kuu. Jaji John Utamwa
aliahirisha kutoa uamuzi mpaka
Jumatatu 06/01/2014
0 comments :
Post a Comment