Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini Tanzania CHADEMA kimewavua uanachama wanachama waandamizi wa chama hicho.
Habari kutoka jijini Dar es Salaam zinasema kuwa, Kamati Kuu (CC) ya CHADEMA iliyokutana katika Hoteli ya Mbezi Garden jijini Dar es Salaam imewavua uanachama aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Dk Kitila Mkumbo, na aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Chama hicho maarufu cha upinzani nchini Tanzania kimekumbwa na mivutano mingi tangu kilipoamua kuwapokonya nyadhifa zote za chama wanachama hao wawili pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe ambaye ameendelea na msimamo wake wa kukituhumu chama hicho kuwa kinaongozwa kwa ubabe.
Siku chache zilizopita, Zitto Kabwe alikimbilia mahakamani nchini Tanzania ili kuzuia Kamati Kuu ya CHADEMA isimjadili na mahakama hiyo ikatoa amri ya kuizuia CHADEMA kumjadili mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini.
CHANZO:IRANI SWAHILI RADIO

0 comments :
Post a Comment