-->

SERIKALI YA ZANZIBAR YAADHIMISHA MIAKA HAMSINI YA MAPINDUZI YA MWAKA 12/1/1964

Zanzibar yaadhimisha miaka 50 ya MapinduziSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hii leo imeadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Muhammed Shein ameongoza sherehe hizo ambazo pia zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mbali na Rais Jakaya Kikwete, marais wa Uganda na visiwa vya Comoro nao wamehudhuria sherehe hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani kisiwani Unguja. Wengine waliohudhuria sherehe hizo ni maseneta kutoka miji ya Lamu na Mombasa Kenya, pamoja na mwakilishi maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China. Akihutubia sherehe hizo, Rais Ali Muhammed Shein wa Zanzibar amewataka wananchi waonyeshe umoja na mshikamano katika sherehe hizo.
Huku hayo yakiripotiwa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, kuwa Siku ya Mapumziko kwa Watanzania wote ikiwa ni kufidia siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyoangukia leo Jumapili. Tangazo hilo limekuja kufuatia tangazo kama hilo lililotolewa na Rais wa Zanzibar kwa wakazi wa visiwa vya Unguja na Pemba.
CHANZO:RADIO IRANI SWAHILI
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment