-->

HII NDIO POST ILIYOZUA MJADALA MKUBWA KWENYE FACEBOOK KUHUSU CHADEMA NA MATUMIZI YA FEDHA

Katika mtandao wa kijamii wa facebook kwenye group moja kubwa sana linaloitwa TANURU YA FIKRA imewekwa post na kijana mmoja aliefahamika kwa jina la Kimea Shembaruku.Post hii imekuwa changamoto kubwa sana kwa wadaupamoja na wanachama wa CHADEMA kwani kila mtu alichangia post hiyo kadri yeye anavyoona.POST yenye hiyo hapo chini:
DONDOO KWA WENYE AKILI ZA SHULE TU.

1. Kurusha Helkopta kutoka Dar-Arusha (Takriban 450KM) kunagharimu takriban 5M, hii ni pamoja na Fuel, parking fees, Mshahara wa rubani na check up.
2. Kurusha helkopta 3 kwa wakati mmoja kuzunguka mikoa 9 (Takriban 4,050KM) kutagharimu zaidi ya 45M
3. Usafiri wa ndani ya mikoa 9 kwa magari, chakula na malazi kwa viongozi kutagharimu takriban TShs laki 5 kwa kila kiongozi mmoja kwa siku.
4. Maandalizi ya sehemu za mikutano, majukwaa, vipaza sauti, umeme na viburudisho kutagharimu takriban TShs laki 5 kwa sehemu moja kwa kila siku moja.
5. Gharama za usalama (Redbigades) mikutanoni, chakula na usafiri vinaweza kugharimu TShs 5,000 kwa kila kijana mmoja kwa siku kwa eneo moja la mkutano.

Inaweza kugharimu chama zaidi ya TShs 600M kwa mzunguko wa mikoa 9 kwa siku chache.

Ni nini vyanzo vya fedha kwa matumizi haya, ruzuku, wafadhili wa ndani/nje au mkopo?

Haya yanafanyika huku chama kikiwa na ofisi za kupanga, huku ofisi nyingine zikiwa zimefungwa kutokana na kushindwa kulipa kodi, Baadhi ya ofisi za mikoa zikitumia magari binafsi ya wanachama waliojitolea huku viongozi wakuu wakisafiri na familia zao kubwa na watumishi wa ndani kwa gharama za chama. AKILI NI MALI, KIJANA USIKUBALI KUTUMIKA NA WANASIASA
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment