MECHI HIYO ILIVUNJIKA KUTOKANA NA KITENDO CHA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA KIISLAM MOROGORO KUFANYA IBADA NDANI YA MAJENGO YA CHUO HICHO CHA JORDAN AMBACHO NI TAWI LA SAINT AGUSTINO KUTOKANA NA KILE WALICHODAI NI UVUNJAJI WA SHERIA KUTOKANA NA KANUNI NA SHERIA ZA CHUO CHAO.WANAFUNZI WA CHUO HICHO CHA JORDAN WALISIKITIKA KWA KITENDO HICHO CHA KUZUIWA KUFANYIKA KWA MECHI HIYO NA KUSEMA KWAMBA PRINCIPAL WAO AMEKUBALI MECHI ICHEZEKE ILA VC WAO NDIO AMEKUWA MGUMU KURUHUSU MECHI HIYO KUFANYIKA.
WANAFUNZI WA MUM WAKISUBIRI USAFIRI WA KUREJEA CHUONI KWAO
WANAMUM WAKIWA BARABARANI TAYARI KURUDI MUM
BUSTANI YA HABARI ILIMTAFUTA COORDITOR WA MCHEZO HUO SANG'ANYA HAMISI RASHIDI NA KUHOJI KUHUSU MAANDALIZI YA MCHEZO HUO NA KUPATA TAARIFA KUWA MCHEZO HUO ULITAKIWA KUCHEZWA IJUMAA YA TAREHE 17/1/2014 ILA WANAFUNZI WA JORDAN HAPO JANA WALIWATAARIFU KWAMBA MECHI HIYO ITABIDI ICHEZWE JUMA TANO KUTOKANA NA WAO KUINGIA KWENYE MITIHANI SIKU YA JUMA TATU.
PIA BUSTANI YA HABARI ILIBAHATIKA KUWAHOJI WACHEZAJI MBALI MBALI WA JORDAN NA KUBAINI KUWA TAARIFA ZA KUBADILISHWA KWA TAREHE YA MECHI HAIKUWA INAFAHAMIKA KATIKA UTAWALA WA CHUO HICHO KWANI HATA JEZI WALIZOVAA WACHEZAJI HAO ZILIKUWA NI JEZI ZA MWAKA WA TATU WA CHUO HICHO.WACHEZJI WA MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO WAWASILI CHUONI KWAO NA KUANZA MAZOEZI MARA TU BAADA YA KUSHUKA KWENYE GARI.
0 comments :
Post a Comment