Kwamujibu wa tarifa zilizo tolewa na makamanda wa
polisi mkoa kusini Pemba kamishina msaidizi swalehe mohamed swalehe na
kamanda wa kikosi cha zima moto na uokozi pemba wamesema ndege hiyo
wakati wa kutua ilipata ikhitilafu ya kufeli breki na kusereka hadi nje
ya uwanja umbali wa mita miambili kwenye vichaka
Wamesema abiria wote wametoka salama hakuna alie
juruhiwa licha ya ndege hio kuacha uwanja kusereka kwenye nyasi na
kungia kwenye mashamba ya muhogo kupita kwenye masiki majiti yalio katwa
nakisha kusimama baada ya ringi kujizonga namizizi ya pori hilo.
Ipo haja kwa mamlaka ya viwanja vya ndege nchini
kutoa taluma kwa watendaji wa kiwanja cha ndege kisiwani pemba kutoa
ushirikiano kwa wandishi wa habari pale inapo tokea dharura kutokana na
watendaji wa kiwanja chandege kisiwani hapa kushindwa kabisa kutoa
usjhirikiano kwa wandishi juu ya tukio hili.CHANZO:ITV
0 comments :
Post a Comment