MTIBWA
Sugar imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa
kirafiki kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania
Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa leo.
Simba
walikuwa wa kwanza kubisha hodi kwenye lango la Mtibwa Sugar kwenye
dakika ya 12 lakini shuti la mshambuliaji mpya wa timu hiyo Ally Badru
liliishia mikononi mwa kipa Hussein Sharif. Kabla ya kupiga shuti hilio
dhaifu Badru alikuwa amepata pasi ya Said Ndemla.
Mtibwa
Sugar walijibu mapigo kwenye dakika ya 25 lakini mshambuliaji wake Jamal
Mnyate alikosa bao la wazi kwa shuti alilopiga kutoka pembeni kidogo ya
lango la Simba.
Timu hiyo
kutoka mkoani Morogoro ilitawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza
nusura wapat bao kwenye dakika ya 27 lakini beki wa Simba Gilbert Kaze
aliokoa mpira uliokuwa unatinga wavuni wa mshambuliaji Masoud Ally.
Simba
walifanya shambulizi la kushtukiza lakini mshambuliaji wake Betram
Mwombeki alipoteza nafasi nzuri ya kufunga kwenye dakika ya 33 akiwa
peke yake na goli lakini shuti lake lilitoka pembeni kidogo ya lango la
Mtibwa Sugar.
Dk 46
Simba walifanya mabadiliko kwa kuwaingiza Nassoro Masoud’Cholo’ na
Adyoun Saleh badala ya Omary Salum na Wiliam Lucian huku Mtibwa
wakifanya mabadiliko kwa kumuingiza Vicent Barnabas badala ya Ally
Mohamedi aliyeumia.
Dk 53
Mtibwa Sugar walipata pigo baada ya mchezaji wake Salim Mbonde kutolewa
nje baada ya kugongana na kipa wake Hussein Shariff na kulazimika
kubebwa kwa machela kupelekwa chumba maalumu cha matibabu.
Dk 65 Ally Masoud aliifungia Mtibwa Sugar bao la kuongoza baada ya kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Hussein Ramadhani.
Vikosi
Simba Yaw Berko. Wiliam Lucian, Omary Salum, Kaze Gilbert, Donald
Musoti, Awadh Juma, Ramadhani Chombo, Edward Cristopher, Betram
Mwombeki, Ally Badru na Saidi Ndemla.
Mtibwa
Hussein Sharif, Said Mkopi, Paul Ngalema, Salim Mbonde, Salvatory Ntebe,
Shaabani Nditi, Ally Shomary, Masoud Ally, Juma Luizio, Jamali Mnyate.
0 comments :
Post a Comment