MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema anamsubiri
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe mahakamani. Zitto ametoa kauli
hiyo siku moja baada ya Mbowe kutangaza kumburuza mahakamani, kutokana
na kile kinachodaiwa kumzushia tuhuma za uongo. “Nasema sitaki malumbano
na kiongozi yeyote, nachotambua masuala ya mahakamani yanajibiwa
mahakamani na si vinginevyo,” alisema Zitto.
Zitto alitoa kauli
hiyo, baada ya waandishi wa habari kutaka kujua msimamo wake kutokana na kauli ya
Mbowe kukusudia kumshitaki, kutokana na madai ya kusema uongo dhidi
yake.
Zitto ambaye yuko nchini Nigeria anakohudhuria vikao vya
Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kwa nchi za Afrika, alisema pamoja
na hali hiyo, mahakama ndiyo njia pekee ambayo haki ya mtu inaweza
kupatikana.
CHNZO:DAR ES SALAAM NEWS LINE
0 comments :
Post a Comment