-->

HAWA NDIO WAJUMBE WA BARAZA KUU AMBAO WATAJADILI MSTAKABALI WA KUREJESHWA KWA VYEO VYA ZITTO KABWE

 
Ni wazi kuwa baada ya Uamuzi wa leo wa Jaji John Utamwa wa Mahakama Kuu ya Tanzania juu ya maombi ya Zitto Kabwe, Zitto anaelekea Baraza Kuu la chama hicho kwa ajili ya kusikiliza rufaa yake ya kuvuliwa nyadhifa zake chamani.

Ni muhimu kujua, angalau, wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA.

Ibara ya 7.7.11 ya Katiba ya sasa ya CHADEMA inaainisha Wajumbe wa Baraza Kuu. Bila ya kuongeza au kupunguza maneno, naona ni vyema nikaiweka hapa kama ilivyo. Inasomeka:...

7.7.11 Wajumbe wa Baraza Kuu la Taifa watakuwa:

(a) Wajumbe wote wa Kamati Kuu.
(b) Wenyeviti wa Baraza la Uongozi, Mikoa.
(c) Wajumbe wateule wasiozidi sita watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa kwa kushauriana na Katibu mkuu na kuidhinishwa na baraza kuu. Wajumbe wateule hawa watateuliwa kwa uwiano wa wajumbe wanne wanaume wawili na wanawake wawili.
(d) Wajumbe watano watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa kila Baraza la Chama, kwa uwiano wa wajumbe wanne toka Bara na mmoja toka Zanzibar kwa kila Baraza.
(e) Wenyeviti wa wilaya za chama
(f) Mwakilishi wa jimbo na chama

Kimsingi, hawa ndio watakaosikiliza na kuamua juu ya rufaa ya Zitto atakapoiwasilisha kwao. Mchakato wa kichama bado unaendelea.
CHANZO:MAARIFA YA JAMII
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment