Waandishi wa habari wanataka Maelezo yangu kufuatia tuhuma lukuki dhidi yangu walizozirejea tena Leo kama kasuku baadhi ya viongozi wa CHADEMA. Jibu langu ni jepesi sana, tuhuma hizo hazipo katika mashtaka dhidi yangu waliyoniandikia wao wenyewe na kunitaka nijibu mbele ya kamati kuu. Kama wanaona tuhuma hizo zina uzito waandike nitoe Maelezo yangu kama mashtaka mapya. Waitishe Baraza Kuu la chama ili lisikie rufaa yangu vinginevyo wakae kimya maana uzushi na kubwabwaja hautawasaidia.
Malicious people are simply manipulative and survive of short term basis. Inspiring people look long term.
KISHA AKAWEKA POST NYINGINE AMBAYO IPO HAPA CHINI
Wakili Tundu Lissu amenituhumu kuwa nimehongwa magari 2 na mheshimiwa Nimrod Mkono. Mimi ninamiliki gari moja mbili, freelnder ninayotumia Dar Es Salaam na Toyota Carina ninayotumia jimboni. Tuhuma hii haimo katika tuhuma nilizotuhumiwa nazo na kuandikiwa na chama ili kujibu. Kama Tundu lissu anadhani tuhuma hii ana ushahidi nayo wa kutosha aiongeze kwenye tuhuma walizoniandikia ili niweze kujitetea kwenye vikao, vinginevyo ni mipasho tu. Nawapa changamoto Tundu lissu na wenzake kama wana tuhuma Mpya dhidi yangu waniandikie kwa mujibu wa taratibu. Tuhuma nilizo nazo hivi sasa na ambazo nimezikatia rufaa katika Baraza Kuu zinahusu mkakati wa kugombea uenyekiti Taifa na kutaka mahesabu ya chama yakaguliwe na CAG.
0 comments :
Post a Comment