'Koplo' feki akichukuliwa maelezo na Luteni Yahya Wangwe na Mteule daraja la pili Albano Semfuko.
Na Mashaka Mhando,TANGA
VIKOSI vya
Ulinzi na Usalama Wilayani hapa, vinamshikilia Edwin John Mponji (31)
kufuatia kwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga na kujitambulisha
kwamba yeye ni koplo wa jeshi la Wananchi JWTZ akitaka kijana wake
afanyiwe mpango wa kuingizwa Jeshi la kujenga Taifa.
"Koplo" Mponji
alikwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Halima Dendego Januari 16
mwaka huu siku ambayo Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani hapa ilikuwa
katika zoezi la kuwafanyia usaili vijana wanaotakiwa kujiunga na jeshi
la kujenga Taifa (JKT).
Akiwa katika
ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Mponji alijitambulisha kuwa yeye ni afisa wa
JWTZ ambaye kwa sasa yupo kikosi cha 36 KJ Mkoani Pwani ambapo
aliambatana na kijana Emmanuel Joseph akitaka afanyiwe mpango ili apate
nafasi.
Hata hivyo
wakati akitoa maelezo hayo,Mshauri wa Mgambo wa Wilaya ya Tanga,Sir Meja
Albano Semfuko alimtilia shaka na kumjulisha Mkuu wa Wilaya ambaye
aliamuru ashikiliwe kwa mahojiano zaidi. Akizungumza na waandishi wa
habari,Mkuu wa Wilaya ya Tanga alisema baada ya mahojiano ilibainika
kuwa Mponji sia askari wa JWTZ ndipo akalazimika kupelekwa nyumbani
kwake mtaa wa Magomeni Jijini hapa alipopekuliwa alikutwa na sare za
JWTZ zikiwa na cheo cha koplo.
Alisema wakati
akikamatwa,Mponji alikuwa amevaa kaptura ya jeshi la Polisi lakini
alipowekwa rumande ya kituo cha Polisi Chumbageni alifanya njama za
kuivua na kisha kumpa mahabusu aliyekuwa akitoka ambaye alitoweka nayo.
Mponji
alionyeshwa kwa waandishi wa habari akiwa amevalia sare ya jeshi la
Wananchi ambapo alipohijiwa alishindwa kutoa maelezo ya kueleweka juu ya
wapi alikokuwa amezipata sare hizo inagawa alikiri kuwa aliwahi
kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kikosi cha 841 KJ Mafinga.
Kufuatia tukio
hilo,Mkuu wa Wilaya ya Tanga aliamuru Jeshi la Wananchi kwa kushirikiana
na Jeshi la Polisi kumfanyia uchunguzi wa kina ili kubaini mtandao
wake.
0 comments :
Post a Comment