-->

WAAFRIKA WAANDAMANA HUKO ISRAEL KUPINGA UBAGUZI WA RANGI UNAOFANYWA NA UTAWALA WA SERIKALI HIYO

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/1578cf2c09a3e8088b3248e346db4f66_XL.jpgMaelfu ya wahajiri wa Kiafrika walifanya maandamano jana mjini Tel Aviv wakipinga siasa za kibaguzi za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wahajiri.
Waandamanaji hao walikuwa wakipinga sharia mpya inayoruhusu vyombo vya usalama kuwafunga wahamiaji wa kigeni kwa kipindi cha mwaka mmoja bila ya kufikishwa mahakamani. Waandamanaji hao pia wameutaka utawala ghasibu wa Israel kuwaachia huru mamia ya wahajiri wa Kiafrika wanaoshikiliwa katika korokoro za utawala huo na kusitisha siasa za kibaguzi za kuwatia nguvuni wahajiri wa Kiafrika.
Jumuiya za kutetea haki za binadamu zinasema kuwa zaidi ya wahajiri mia tatu wametiwa nguvuni tangu Bunge la Israel lipasishe sheria inayoviruhusu vyombo vya usalama kuwashikilia wahajiri wa kigeni kwa muda mrefu.
Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umekosoa vikali siasa za utawala wa kibaguzi wa Israel dhidi ya wahajiri wa Kiafrika hususan sharia inayotumiwa na utawala huo dhidi ya wahajiri. Taarifa iliyotolewa na Kamisheni Kuu ya Umoja wa Mataifa inahushughulikia masuala ya wakimbizi imesema siasa hizo za Israel zinapingana na makubaliano ya mwaka 1951 ya Geneva kuhusu wakimbizi
CHANZO:IRANI SWAHILI R
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment