-->

UNDANI KUHUSU TAARIFA YA KUJIUZULU KWA JOHN MNYIKA

Jana mitandao ya kijamii ilijazwa
taarifa kwamba jana jioni, John
Mnyika (Mb) alimwandikia barua ya
kujiuzulu Katibu  Mkuu wa CHADEMA.
Ofisa Habari Mwandamizi wa
CHADEMA, Tumaini Makene (0752
691569) alijibu kwa kukanusha kuhusu
taarifa hizo na kuongeza kuwa kwa
muda uliotajwa, Mhe. Mnyika
alikuwa katika shughuli za chama
akitimiza majukumu yake.
Akasema taarifa hizo ni mradi wa
kutengeneza uongo unaofadhiliwa na
watu kwa sababu ya, “kuwasumbua
wanachama na
Watanzania, lakini pia kutaka
kuonesha kuwa kundi la wasaliti na
wanafiki ndani ya chama linaungwa
mkono na watu makini ndani ya
chama ambao kama wangekuwa
upande wao, wangesaidia kundi hilo
kuondoa taswira hasi linalopata
mbele ya jamii. Wanatafuta uhalali
walioupoteza kwa kufanya harakati za
kusaliti mapambano.
Mioyoni mwao wanaumia kweli kweli
kuonekana wanaungwa mkono na
watu wasio wanachama wa
CHADEMA, ambao wengine
wanalazimika kwenda kuwanunua
pale feri Posta na Kariakoo ili waje
kuwashangilia Mahakamani na
kukimbia barabarani.
Tunajua wanaumia kutumia mamilioni
kukodi watu kuja kulia kwenye msiba
wasioujua wala usiokuwa wa kwao,
huku wakidai ujira hadharani.”
aliandika Makene kwenye tovuti ya
MwanaHalisiForum
Kubenea katika tovuti hiyo
aliandika, “Nathibitisha ifuatavyo:
Nimeonge na Mnyika muda huu,
amenihakikishia kuwa habari hiyo siyo
ya kweli. Hajajiuzulu na wala hana
sababu ya kujiuzulu. Anasema,
hawezi kuungana na watu
wanaokivuruga chama. Anaipenda
Chadema na anaamini ndiyo chama
bora kwa sasa.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment