-->

SHEKH ILUNGA AKAMATWA NA KUACHIWA KWA DHAMANA TABORA

Shekh Ilunga Hassan Kapungu inasemekana hapo jana alikamatwa na polisi kisha kupekwa kituoni huko mkoani Tabora.Shekh Ilunga alikuwa anakabiliwa na kesi ya kutoa CD zilizodaiwa kuwa ni za uchochezi,Tangazo la kutafutwa kwa Shekh Ilunga lilikuja mwezi wa nne wakati Shekh Ilunga akiwa India akipatiwa matibabu.
Katika kesi hiyo ya kutoa CD/DVD za uchochezi alikuwa pamoja na Askofu Mpemba,Imam Hamza pamoja na Shekh Ilunga,Imam Hamza alifunguliwa mashtaka mahakamani ila Askofu Mpemba pamoja Ilunga ambao ilisemekana kutokuwepo nchini kipindi agizo hilo la kukamatwa kwao linatolewa.Askofu Mpemba ilisemekana kuwa yupo Marekani na Shekh Ilunga alikuwa India alipokuwa anapatiwa matibabu(mzizima24).
Kanda zilizopigwa marufuku ni pamoja na  
Unafiki katika SensaBakwata tawi la Kanisa,Mauaji ya Sheikh Abdu Rogo wa Mombasa na Mwisilamu rudisha Imani zilitolewa na Sheikh Ilunga, Ndege wote walie akilia Bundi Uchuro ya Imamu Omary na Inuka chinja ule iliyotolewa na kusambazwa na Askofu Mpemba.
Shekh Ilunga ambae imesemekana kurejea nchini kutokea nchini India alipokuwa anapatiwa matibabu alikamatwa jana na kupelekwa kituoni na baadae kuachiwa kwa dhamana.
Mpaka sasa bado haijafahamika hatma ya  Askofu Augustine Mpemba wa Kanisa la Tanzania Field Evangelist na Mkurugenzi anayemiliki kituo cha Redio Kwa Neema FM cha Jijini Mwanza ambacho kilifungiwa na TCRA miezi sita kwa ukiukwaji wa maadili ingawaje inasemekana yupo nchini na anasikika kwenye kituo hicho cha Radio Kwa Neema mara kadhaa.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment