-->

NDEGE ZISIZO NA RUBANI ZA MAREKANI ZAUA NCHINI YEMEN

Watu 17 wameuawa  wakati ndege ya kivita ya Marekani isiyo na rubani (drone) iliposhambulia  msafara wa harusi kusini mwa Yemen.
Hujuma hiyo imejiri Alkhamisi katika mkoa wa al Bayda na maafisa wa usalama wanasema  kombora lililenga gari lililokuwa katika msafara wa harusi na kwamba watu 10 waliuawa papo hapo na wengine saba walipoteza maisha wakiwa hospitalini.
Watu wengine kadhaa wamejeruhiwa katika tukio hilo ambalo ni dhihirisho la kuendelea jinai za Marekani dhidi ya raia wasio na hatia.
Marekani imekuwa ikitumia ndege hizo zisizo na rubani kushambulia maeneo mbalimbali ya nchi za Kiislamu kama Somalia, Afghanistan, Yemen na Pakistan kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. Aghalabu ya wanaopoteza maisha katika hujuma za ndege hizo za Marekani ni raia wa kawaida wakiwemo wanawake na watoto wasio na hatia.http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/3278e257e1f7e19221f73c4a0e6de949_XL.jpgCHANZO:SWAHILI IRANI
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment