Aida
Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya,
hivi karibuni alijifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo(Quadliplets)
katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu
katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua
majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika
Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na
matarajio ya Wengi. SOMA ZAIDI MBEYA YETU BLOG
0 comments :
Post a Comment