-->

MAENDELEO YA UTAFUTAJI WA NDEGE ILIYOPOTEA YAGONGA MWAMBA

Malaysia-Airlines-Boeing-B777-200-Flight-MH370

Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia, Warren Truss, kulia, akizungumza na ofisa wa juu ya kikosi cha uokoaji na mratibu wa operesheni ya kuitafuta ndege iliyopotea, John Rice. Wataalamu wa Rada wakiwa wamepigwa picha ndani ya ndege ya Kijeshi ya New Zealand wakiwa katika msako wa chombo hicho kilichopotea Kusini mwa bahari ya Hindi.
Mmoja wa wanajeshi wa kikosi cha maji cha China akiwa ndani ya meli Snow Dragon, wakiendelea na msako wa ndege iliyopotea kusini mwa bahari ya Hindi.
Mike Barton, mkuu wa kikosi cha uakoaji, kushoto, akiangalia ramani ya Bahari ya Hindi akiwa na Alan Lloyd, ofisa wa kitengo cha uokoaji katika Jeshi la Majini la Australia.
Ndugu wa abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo, raia wa China wakilia na wengine kupatwa na mshangao baada ya kuendelea kuripotiwa habari za kutojulikana ilipo ndege hiyo, wakati wakiongea na waandishi wa habari mjini Beijing.
Naibu Waziri Mkuu wa Australia Warren Truss akizungumza na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya utafutwaji wa ndege iliyopotea. 


NDEGE ya abiria ya Malaysia iliyopotea kiutatanishi wiki mbili zilizopita, inadaiwa iliruka chini ya futi 12,000 kutoka usawa wa bahari kutokana na matatizo katika chumba cha rubani kabla ya kupotea katika rada, ripoti mpya zimeeleza. 


Wakati ndege hiyo Boeing 777-200 ikiwa bado inatafutwa katika bahari ya Hindi, habari zinasema chombo hicho kilibadili uelekeo ikiwa juu ya bahari ya Kusini ya China.

Mara ya mwisho ndege hiyo ilionekana katika rada ya jeshi la Malaysia saa 2.15 asubuhi kwa saa za nchi hiyo, Machi 7 mwaka huu, ikiwa katika kisiwa cha Penang kilicho kusini mashariki mwa taifa hilo, muda kama saa moja baada ya kuwa imeruka kutoka Kuala Lumpur kwenda Beijing nchini China.


Mapitio ya Rada yalionyesha ndege hiyo ikibadili mwelekeo baada ya kugeuka ghafla na kwa kasi upande wake wa kushoto kuelekea Malacca.


Ofisa mmoja aliyekataa kutajwa jina kwa vile siyo msemaji, aliiambia CNN kwamba kuruka chini ya futi 12,000 katika anga yenye ndege nyingi kama ilipokuwa ikipita kungeifanya ndege hiyo kutoonekana na ndege zingine.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment